Habari mpya

PERUZI HABARI MBALI MBALI ZA ULIMWENGU LEO JULY 8, 2016..

 
Rais Barack Obama ashutumu mauaji ya Wamarekani weusi na walipuaji wa kujitoa mhanga washambulia sehemu takatifu kwa Waislamu wa Kishia nchini Iraq.

1. Obama shutumu mauaji ya weusi Marekani


Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa tukio la kupigwa risasi kwa raia wawili Wamarekani weusi na maafisa wa polisi, mara kwa mara, sio visa vya kipekee, na kwamba raia wote wa Marekani wanafaa kutamaushwa.
Gavana wa Minnesota, amesema hadhanii kuwa afisa wa polisi angempiga risasi dereva, ambaye alitolewa kutoka ndani ya gari ambalo mojawepo ya taa yake ya nyumba ilikuwa imevunjika, kama angelikuwa ni mtu mweupe.
Huku hayo yakijiri habari za hivi punde kutoka Marekani, zasema kuwa maafisa wanne wa polisi wamepigwa risasi katika mji wa Dallas nchini humo.

2. Eneo takatifu kwa Washia lashambuliwa Iraq


Walipuaji wa kujitoa mhanga wameshambulia sehemu takatifu kwa waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, katika maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu Baghdad.
Bomu moja lililipuka katika lango la kaburi la Sayid Mohammed bin Ali al-Hadi, katika mji wa Balad. Baada ya mlipuko huo, watu kadhaa waliokuwa na silaha, walianza kuwamiminia risasi waumini waliokuwa wakiadhimisha siku kuu ya Eid.
Baadhi ya washambuliaji walijilipua. Zaidi ya watu 30 wamethibitishwa kufariki.

3. Wapakistani 12 wakamatwa Saudi Arabia


Wakuu nchini Saudi Arabia wamewatia mbaroni washukiwa 19, 12 kati yao wakiwa raia wa Pakistan kuhusiana na shambulio la bomu la kujitoa mhanga, katika msikiti wa Nabii mjini Medina, hapo siku ya Jumatatu.
Msemaji wa serikali amesema kwamba, mlipuaji wa kujitoa mhanga, alikuwa na umri wa miaka 26 raia wa Saudia, ambaye alikuwa mtumiaji wa dawa za kulevya.

4. Kamanda wa zamani wa jeshi Chile atiwa mbaroni


Kamanda wa zamani wa jeshi la Chile, Jenerali Juan Emilio Cheyre, amezuiliwa kwa kudaiwa kuhusika katika mauaji ya watu 15, baada ya tukio la mapinduzi lililotendeka mnamo mwaka 1973. Operesheni yake ilikuwa sehemu ya mauwaji mabaya yaliyopewa jina "Caravan of Death" (Msafara wa Mauti) --yaliyotekelezwa na idara hatari ya kijeshi.
Idara hiyo ilibuniwa na Jenerali Pinochet na kuwekwa maeneo ya vijijini nchini Chile, ili kuwasaka, kuwakamata na kuwaua wakereketwa wa upinzani.

5. Watu 20 wajeruhiwa kwenye treni Taiwan


Maafisa wakuu nchini Taiwan wanasema kuwa zaidi ya watu 20 wamejeruhiwa, katika mlipuko wa bomu ndani ya treni moja ya abiria katika mji mkuu Taipei.
Polisi wanashuku kuwa mlipuko huo umetokana na bomu la bomba.

6. Utafiti: Wengi wameridhishwa na Obama


Na utafiti uliofanywa na shirika la Habari la BBC, umebaini kuwa zaidi ya asilimia sabini ya watu, wamefurahia utendakazi wa Rais Barrack Obama katika muhula wake wa pili uongozini.
Kati ya mataifa 19 ya waliohojiwa, ni Urusi tu ndilo taifa ambalo lilikuwa na mtazamo hasi, ya urais wa Obama, huku ikiwa tu na asilimia 18 ya wanaopenda utawala wake.

No comments

+255716829257