AUDIO: JERRY MURO AFUNGUKA HAYA BAADA YA TFF KUTANGAZA KUMFUNGIA MWAKA MMOJA..

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano waYanga Jerry Muro jioni ya July 7 2016 ameingia kwenye headlines baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya maadili, kutangaza kumfungia mwaka mmoja kujihusisha na soka na faini ya Tsh milioni 3.
Jerry Muro amefungiwa na kamati ya maadili kwa makosa mawili, moja alilifanya mwaka 2015 la kukaidi kulipa faini ya Tsh milioni 5 iliyoamuliwa kulipa na kamati ya nidhamu baada ya kufanya makosa, kosa ambalo limemfanya afungiwe mwaka mmoja kujihusisha na soka.
Kosa la pili ni kutuhumiwa kuchochea vurugu kuelekea mchezo wa Yanga wa Kombe la shirikisho dhidi ya TP Mazembe uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, baada ya hukumu hiyo kutoka Jerry Muro kutoka Machame Kilimanjaro aliyazangumza haya..

“Taarifa hizo nimezisikia japo kwa sasa nipo kijijini Machame kwa ajili ya likizo yangu, nimesikia watu wameandika kwenye mitandao kuwa nimefungiwa, lakini mimi nipo Machame na maamuzi yao yametoka nikiwa likizo Machame, yaani wametoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja”
Sikiliza sauti ya Muro hapa chini..
Sikiliza sauti ya Muro hapa chini..
chanzo: millardayo.com
No comments
+255716829257