Habari mpya

BALOTELLI ATAKIWA KUONDOKA LIVERPOOL..

 
 Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema mshambuliaji Mwitaliano Mario Balotelli anafaa kutafuta klabu mpya.
Balotelli, 25, alikaa AC Milan kwa mkopo msimu uliopita lakini amerejea Liverpool kwa mazoezi ya kabla ya msimu.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City amefungia Liverpool mabao manne tangu ajiunge nao 2014.
“Hayumo katika kiwango cha uchezaji ambapo anafaa kuwa akishindania nafasi moja au mbili na wachezaji wane au watano,” amesema Klopp.
“Kwa hivyo, ni wazi kwamba tunahitaji suluhu. Kutakuwa na klabu ambayo itakuwa na furaha kuwa na Mario Balotelli mpya."

No comments

+255716829257