Habari mpya

Ibrahimovic huenda akose mechi Uchina

 Ibra
 Meneja mpya wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anapanga kutosafiri na mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic Uchina.
Mourinho hata hivyo amepanga kuwachukua wachezaji wa England Wayne Rooney, Chris Smalling na Marcus Rashford.
Klabu hiyo inapanga kucheza mechi mbili za kujiandaa kwa msimu ujao na inapangiwa kuwasili Uchina Jumanne.
Mourinho amesema Rooney, Smalling na Rashford hata hivyo hawatacheza dhidi ya Borussia Dortmund mjini Shanghai tarehe 22 Julai na Manchester City mjini Beijing mnamo 25 Julai.
Ibrahimovic, 34, huenda asishirikishwe hata kidogo.
Akikosa kusafiri na timu hiyo bara Asia, basi mashabiki watasubiri muda zaidi kumtazama Ibrahimovic akicheza mechi yake ya kwanza United.
United wanatarajiwa kucheza dhidi ya Salford City uwanjani Moor Lane mnamo 26 Julai.
Mechi hiyo ilipothibitishwa, Gary Neville, mmiliki mwenza wa Salford aliandika kwenye Twitter: "Mechi ya kwanza kwa Zlatan!!"
United baadaye watacheza dhidi ya Galatasaray mjini Gothenburg nchini Sweden, nchi anamotoka Ibrahimovic tarehe 30 Julai.
Kisha, watakutana na Everton mechi ya heshima kwa Wayne Rooney Old Trafford mnamo 3 Agosti kabla ya kukutana na mabingwa wa Ligi ya Premia kwa mechi ya Community Shield mnamo 7 Agosti.

No comments

+255716829257