Habari mpya

WATAKAO TUMBUIZA KWENYE BET AWARDS JUNE 26, 2016 HAWA HAPA...

Future, Usher, na Bryson Tiller wametangazwa kuongezwa kwenye orodha ya wasanii watakaotumbuiza siku hiyo. Wanaungana na mastaa wengine waliokuwa wametangazwa awali ambao ni pamoja na Alicia Keys, Maxwell, pamoja na tribute ya Prince itakayotolewa na D’Angelo, The Roots na Janelle Monáe.

Mastaa watakaokabidhi tuzo ni pamoja na DJ Khaled, Gabrielle Union, Tinashe, Fantasia, Regina Hall, Birdman, Jermaine Dupri, Dame Dash na Snoop Dogg.
Diamond ni miongoni mwa wasanii wanaowania tuzo hizo mwaka huu kwenye kipengele cha Best International Act: Africa.
Washereheshaji wa show hiyo watakuwa ni Anthony Anderson na Tracee Ellis Ross.
Tuzo hizo zitatolewa June 26 live kutoka Microsoft Theater, Los Angeles, Marekani.
chanzo: Beka boy

No comments

+255716829257