SERIKALI YAAZIMIA KUWAKOMBOA VIJANA WAHITIMU KATIKA JANGA LA AJIRA..
NA CHAUYA ADAMU.
Kufuatia uhaba wa ajira nchini, serikali kwa
kushirkiana na mashirika binafsi imeazimia kutoa mikopo kwa vijana hasa
wanaomaliza vyuo vikuu badala ya kusubiri ajira za mojakwamoja kutoka
serikalini.
Alipozungumza na vijana katika semina ya
ujasiriamali iliyoandaliwa na jukwaa la jamii ya wajasiriamali Tanzania (TASEF),
ofisa maendeleo kutoka wizara ya sera, bunge, kazi ajira na vijana ofisi ya
waziri mkuua, Godfrey Chacha, amesema katika mchakato wa kupunguza umasikini
nchini, serikali kwa kushirikiana na mashirika binafsi imeamua kutoa ajira kwa
vijana ili kutatua tatizo la ajira nchini.
“Vijana wanalia na tatizo la ajira kila siku,
serikali imeamua kuchukua jukumu la kuwapa mikopo amabayo itawasaidia
kujiajiari wenyewe badala ya kusubiri ajira za mojakwamoja” alisema Chacha.
Chacha ameongeza
kuwa mikopo itatolewa kupitia vikundi ambapo vijana wametakiwa kubuni mawazo ya aina gani ya biashara
watakayoifanya.
Hata hivyo amesema kila kikundi kinatakiwa kuwa na
usajili ambapo kitaandika barua ya maombi kwenda kwa afisa mtendaji wa kata
kwaajili ya utambulisho ambayo itapelekwa mojakwamoja hadi kwa afisa maendeleo
wa wilaya au manispaa.
“Mnatakiwa kutengeneza vikundi vyenye usajili kutoka
katika halmashauri au manispaa zenu ambapo mtaandika barua za kuomba mkopo huo
mkiambatanisha na aina gani ya biashara mtakayofanya”
“hakikisheni mnakuwa na pendekezo (proposal) pamoja
na jina la kikundi katiba ambavyo amabapo baada kupata barua kwa mtendaji kata,
mtapeleka kwa afisa maendeleo wa wilaya au manispaa na hapo itafika wizarani”
Alisema Chacha.
Chacha amesema
serikali itatoa milioni kumi kwa kila kikundi chenye sifa ambapo itakata riba
ya asilimia kumi maada ya muda wa miaka miwili.
Kwa upande mwingine, shirika linalosaidia kutatua
changamoto za watoto barani Africa (Reach for Change Africa) limesema
linahitaji kupata mawazo chanya kutoka kwa vijana juu ya namna ya kuwasaidia
watoto nchini, amabapo kupitia ushindani litatoa Milioni arobaini kwa kila
mshindi lengo ikiwa ni kuwasaidia vijana kutatua tatizo la ajira kupitia
ujasiriamali.
Redemtha William
ni (program assistance) katika shirika hilo, amesema shirika lao linawasidia
vijana wasio na ajira kwa kupokea mawazo yao ambayo yatasaidia kutatua
changamoto za watoto katika jamii.
“Katika
kupambana na umasikini tumeungana na serikali kuwapatia vijana mitaji kwaajili
ya ujasiriamali amabapo tunahitaji wawe wagunduzi kwa kuja na mawazo yatakayo saidia kutatua
changamotomo za watoto katika jamii”
Hata hivyo washiriki wa semina hiyo wamesema tatizo
kubwa kwa vijana si swala la ajira pekee lakini ni namana gani ya kuiendesha
ajira hiyo amabapo wameiomba serikali kuandaa mafunzo kwa vijana juu ya
ujasiriamali kabla ya kuwapa fedha hizo.
Dickson Edward, mhitimu wa chuo cha ustawi wa jamii,
amesema kwa kuwa serikali imeshindwa kuwaajiri vijana, kuna ulazima wa kuandaa
mafunzo na kozi maalum za ujasiriamali tangu wakiwa chuoni
“Ni wazi kabisa serikali imeshindwa kuwaajiri
wahitimu wote wa vyuo vikuu lakini kuna tatizo lingine la vijana kushindwa
kuajirika, nadhani kuna umuhimu wa serikali kuandaa mafunzo maalum kwa vijana
juu ya ujasiriamali tangu wakiwa vyuoni” alisema Dickson
Dickson ameongeza kuwa serikali lazima irekebishe
mitaala vyuoni na hivyo masomo ya ujasiriamali yapewe kipaumbele ili kuwajenga
vijana kuwa wajasiriamali.
Kutokana na mlolongo mrefu wa upatikanaji wa mikopo
hiyo, Happiness Njovu mhitimu wa chuo kiuu Tumaini tawi la Dar es salaam
amesema serikali ipunguze mlolongo huo kwani ni mrefu na utachukua muda
kupatikana kwa mikopo hiyo.
“Fikiria utunge katiba, ufanye usajiri, uandike barua ya
maombi kwa mtendaji, uende kwa afisa maendeleo wa wilaya, aipeleke mkoani ndiyo
ifike wizarani, huo mkopo utachukua muda kupatikana na na unaweza usipate
kabisa”
“ni bora watengeneze fomu maalum tujaze watupatie
mkopo kama wana nia ya dhati kutusaidia” alisema Happiness.
No comments
+255716829257