MAREKANI YATOA POLE KWA UTURUKI KUFUATIA SHAMBULIO LA MABOMU..
Rais wa Marekani Barack Obama
amemwambia Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoÄŸan kuwa nchi ya Marekani
ipo pamoja na watu wa Uturuki katika wakati huu mgumu baada ya
kushambuliwa kwa uwanja wake wa ndege wa Istanbul kwa mabomu ya kujitoa
muhanga siku ya Jumanne.
Maafisa nchini Uturuki wanaamini kuwa
wanamgmbo wa IS walihusika katika shambulizi hilo lililouwa zaidi ya
watu 40 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.Obama anasema kuwa amempigia simu Rais wa Uturuki kumpa salam za rambirambi sambamba na kusisitiza dhamira ya nchi yake kuendeleza mapigano dhidi ya IS.
Shambulio hilo linatajwa kuwa limeuwa watu wengi zaidi nchini humo ikilinganishwa na mashambulizi kadhaa yaliyopita.
No comments
+255716829257