Habari mpya

EURO: WABELGIJI MACHO YOTE KWA HAZARD..

 Hazard
Timu ya taifa ya Ubelgiji inasubiri kwa muda kubaini iwapo mchezaji matata Eden Hazard ataweza kuwachezea mechi muhimu ya Euro 2016 dhidi ya Wales Ijumaa.
Hazard, 25, mshambuliaji wa Chelsea, alifunga bao kwa ustadi mkubwa wakati wa mechi waliyoshinda 4-0 dhidi ya Hungary hatua ya muondoano.
Hata hivyo, aliumia paja wakati wa mechi hiyo na hajashiriki mazoezi tangu wakati huo.
"Tunafanya kila juhudi kuhakikisha yuko asilimia 100 sawa kucheza,” amesema meneja wa Ubelgiji Marc Wilmots.
"Siwezi nikawapa hakikishe kuhusu ni wakati gani hili litafanyika, na pia siwezi nikawathibitishia kwamba atakuwa sawa.”
Vijana hao wa Wilmots, walioorodheshwa nambari mbili kwa ubora duniani, walicheza dhidi ya Wales wakati wa mechi za kufuzu kwa Euro 2016 na Kombe la Dunia 2014.
Walishindwa mechi zote tatu walizocheza karibuni zaidi.
Mechi ya karibuni zaidi Wales walishinda 1-0 mjini Cardiff Juni 2015.

No comments

+255716829257