Romelu Lukaku alifunga mabao mawili
huku timu ya taifa la Ubelgiji ikipata ushindi wake wa kwanza katika
michuano ya Euro2016 na kuharibu fursa ya timu ya Jamhuri ya Ireland
kufika robo fainali.
Baada ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza
ambapo hakuna timu ilioona lango la mwengine,Lukaku aliifungia Ubelgiji
bao la kwanza baada ya kupata pasi muruwa.Baadaye Axel Witsel alifunga bao la pili kupitia
kichwa katika dakika ya 61,kabla ya Lukaku kufunga bao la tatu baada ya
kushambulia ngome ya Ireland.
EURO: UBELGIJI YAICHAPA JAMHURI YA IRELAND 3-0..
Reviewed by Chimbuko Online
on
June 19, 2016
Rating: 5
No comments
+255716829257