Habari mpya

Sayari ya Utaridi kuonekana ikipita kwenye jua

UtaridiImage copyrightScience Photo Library
Image captionTukio kama la leo lilishuhudiwa miaka kumi iliyopita
Sayari ya Utaridi, ambayo ndiyo ndogo zaidi miongoni mwa sayari zinazolizunguka, leo itaonekana katikati mwa jua na dunia.
Tukio hilo litadumu saa saba na hutokea njia ya Utaridi, inayojulikana pia kama Zebaki, kulizunguka jua na njia ya dunia kulizunguka jua zinapolingana.
Tukio hilo hufanyika mara 13 au 14 kila karne na mara nyingine kutokea itakuwa 2019, na baadaye 2032.
Miaka ya nyuma, tukio hilo lilionekana 2006, 2003 na 1999
Wataalamu wa astronomia wanasema kwa kutegemea hali ya anga, tukio hilo litaonekana vyema zaidi maeneo ya magharibi mwa Ulaya, kaskazini na magharibi mwa Afrika, kaskazini mashariki mwa Amerika na maeneo mengi ya Amerika Kusini.
Tukio hilo litatokea mwendo wa saa nane na dakika kumi na mbili adhuhuri saa za Afrika Mashariki.
Sayari ya Utaridi, inayokaribia jua zaidi, huwa na joto kali, kiwango chake cha joto kikiwa mara sita kushinda maeneo yenye joto zaidi duniani wakati wa mchana.
Usiku, sayari hiyo huwa na baridi kali.
Kwa sababu Utaridi ni sayari ndogo sana, tukio la leo litaonekana vyema tu kwa kutumia darubini na watu pia wanashauriwa kutumia darubini zenye kifaa cha kupunguza miali ya jua ili kukinga macho.
Chanzo: BBC

No comments

+255716829257