Habari mpya

JUMBA JINGINE LAPOROMOKA KENYA..

Jumba
Image captionMaafisa wa serikali wamefika eneo hilo
Sehemu ya jumba kubwa la kibiashara mjini Mombasa imeporomoka siku chache baada ya jumba la makazi kuporomoka jijini Nairobi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.
Sehemu ya jumba hilo la Nyali Centre iliporomoka usiku wa kuamkia Jumatatu.
Hakuna aliyeripotiwa kujeruhiwa wakati wa mkasa huo.
Jumba la Nyali Centre huwa na kituo cha mazoezi na mgahawa maarufu.
Polisi, maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu na maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Ujenzi (NCA) wamefika eneo hilo kufanya uchunguzi zaidi.
CHANZO: BBC

No comments

+255716829257