Habari mpya

PERUZI HABARI KUU ULIMWENGUNI LEO MEI 12..

Miongoni mwa habari kuu leo, Donald Trump amelegeza msimamo kuhusu Waislamu, maseneta Brazil wanajadili kumtoa madarakani Dilma Rousseff.

1. Trump alegeza msimamo kuhusu Waislamu

Image copyright
Mgombea wa tiketi ya chama cha Republican katika uchaguzi wa urais nchini Marekani Donald Trump ameonekana kulegeza msimamo wake kuhusu mpango wa kuwazuia Waislamu kuingia Marekani kwa muda ikiwa atachaguliwa kuwa rais. Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Fox News, Trump amesema tamko lake lilikuwa ni pendekezo tu na kwamba bado wito haujatolewa kulitekeleza.

2. Bunge lajadili kumtoa madarakani Rousseff

RousseffImage copyrightAP
Image captionWanaomuunga mkono Rousseff wameandamana
Kikao maalum cha bunge la Senate nchini Brazil kujadili ikiwa rais wa taifa hilo Dilma Rousseff aondolewe madarakani au la kimegeuka na kuwa ulingo wa hatuba ndefu.
Wengi wa waliohutubia kikao hicho wameunga mkono kuanzishwa mchakato wa kumuondoa Bi Roussef madarakani, wakimshutumu kwa kuvunja sheria za mapato ya serikali na kusimamia vibaya uchumi wa taifa hilo.

3. Wafanyakazi Nigeria wapinga hatua ya serikali

BuhariImage copyrightGETTY
Image captionRais Buhari yumo nchini Uingereza
Chama kikuu cha wafanyikazi nchini Nigeria kimesema kuwa kitapinga hatua ya serikali kupunguza ruzuku ya mafuta ambayo huenda ikasababisha bei ya bidhaa hiyo muhimu kuongezeka maradufu.
Chama hicho cha Nigeria Labour Congress kimetaja mpango huo kuwa usio na sababu na wa kihalifu.
Jaribio la kupunguza ruzuku ya mafuta mwaka 2012 lilisitishwa baada ya kuzuka maandamano makubwa yenye vurugu pamoja na migomo.

4. Marekani kuunga mkono pendekezo la UN

Image copyrightAP
Marekani imetoa ahadi ya kuunga mkono kanuni zitakazowaruhusu wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa kuchukua hatua za kijeshi kuwalinda raia wakati wowote ikiwa patatokea vita.
Kanuni hizo zilizopewa jina la Kanuni za Kigali ziliafikiwa nchini Rwanda mwaka uliopita, baada ya taifa hilo kutelekezwa na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

5. Nissan kununua hisa za Mitsubishi

Image copyrightOTHER
Kampuni za utengenezaji magari za Mitsubishi na Nissan nchini Japan, zimethibitisha kuwa zinafanya mazungumzo ya kuingia mkataba wa kifedha.
Mitsubishi inakabiliwa na wakati mgumu baada ya sakata ya udanganyifu kuhusu takwimu za kasi ya matumizi ya mafuta katika magari yake.
Vyombo vya habari nchini Japan vimesema kuwa Nissan itachukuwa theluthi moja ya mtaji wa kampuni ya Mitsubishi na hivyo kuwa kampuni kubwa zaidi inayomiliki hisa nyingi katika kampuni hiyo.

6. Visa vya utoaji mimba vyashuka

Image copyrightAFP
Na utafiti mpya umebaini kuwa viwango vya uavyaji mimba vimeshuka kwa kiwango kikubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika historia ya mataifa yaliyostawi, hali iliyochangiwa na kuboreshwa kwa viwango vya huduma za uzazi wa mpango.
Katika mataifa yanayoendelea, ambako huduma hizo hazipatikani kwa urahisi visa vya uavyaji mimba vimeendelea kuongezeka.
CHANZO: BBC

No comments

+255716829257