Habari mpya

Marekani yakumbatia mageuzi kwa walinda amani UN

UNImage copyrightAP
Image captionMapendekezo hayo yanawapa wanajeshi wa UN mamlaka zaidi ya kulinda raia
Marekani imeahidi kuunga mkono mapedekezo mapya yanayolenga kuwapa wanajeshi walinda amani wa Umoja wa Mataifa mamlaka zaidi.
Wanajeshi hao watapata ruhusa ya kuchukua hatua madhubuti kulinda raia kwa urahisi wakati wa mizozo ya kivita.
Mapendekezo hayo, yanayofahamika kama Kanuni za Kigali, yaliafikiwa mwaka jana nchini Rwanda, taifa ambalo lilitelekezwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Umoja wa Mataifa ulisema kwenye ripoti ya mwaka 2014 kwamba katika miaka minne iliyotangulia, walinda amani wa umoja huo walishindwa kutumia nguvu kulinda raia katika visa karibu 500 vya mashambulio.
Nchi 29 kufikia sasa zimetia saini kanuni hizo lakini nchi nyingi zinazochangia wanajeshi walinda Amani wa UN zikiwemo India na Pakistan hazijatia saini kanuni hizo.
Kadhalika, nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama vile Uingereza na Ufaransa hazijaukumbatia.
CHANZO: BBC

No comments

+255716829257