Habari mpya

MZOZO WA DENI WAZUIA NDEGE YA MSWATI NCHINI CANADA..

Image copyrightAFP
Image captionMfalme mswati ana wake wengi
Ndege ya kibinafsi ya mfalme wa Swaziland Mswati wa tatu, imezuiwa nchini Canada kwa mara ya pili ndani ya miaka miwili kutokana na mzozo wa deni.
Ndege hiyo ilizuiwa kama sehemu ya kesi iliyo mahakamani, iliyowasilishwa na aliyekuwa mfanyibiashara mwenza wa mfalme Mswati raia wa Singapore Shanmuga Rethenam, ambaye anasema kuwa anaudai ufalme wa Swaziland kima cha dola milioni nane.
Siku ya Jumatano msemaji wa serikali ya Swaziland Percy Simelane, alikana madai kuwa mfalme ana deni lolote na kuongeza kuwa hatasema zaidi kwa kuwa kesi iko mahakamani.
CHANZO: BBC

No comments

+255716829257