Habari mpya

MKUTANO WA WAKUU WA MAJESHI YA AFRIKA KUMALIZIKA LEO JIJINI ARUSHA..

Mkutano wa wakuu wa Majeshi ya nchi kavu Afrika kujadili changamoto zinazoyakabili majeshi hayo unamalizika leo, jijini Arusha.
Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi, Luteni Kanali Ngeleba Lubinga, viongozi hao wamepeana uzoefu wa kukabiliana na ugaidi, mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu, ikiwemo usafirishaji watoto pamoja na dawa za kulevya.
Mkutano huo, ulioanza Mei 16 na Kufunguliwana Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi, umewashirikisha wakuu wa majeshi ya nchi kavu zaidi ya 38.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257