Habari mpya

MWANAMKE AHOFIWA KULIWA NA MAMBA AUSTRALIA..

Image copyrightAP
Image captionMamba
Polisi kaskazini mwa Australia wanasema kuwa mwanamke mmoja hajulikani aliko, baada ya kushambuliwa na mamba alipokwenda kuogelea usiku.
Mwanamke huyo na rafiki yake walikuwa katika kidibwi chenye kina kifupi katika hifadhi ya kitaifa ya wanyama pori ya Daintree.
Hifadhi hiyo ya taifa ipo katika maeneo ya Queensland, nchini humo.
tukio hilo ni limetokea Jumapili jana, ambapo hadi sasa inahofiwa kuwa huenda ameliwa na Mamba.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257