Sakho apewa marufuku ya siku 30 na Uefa
Beki wa Liverpool Mamadou Sakho amepewa marufuku ya siku 30 na shirikisho la soka barani Ulaya Uefa baada ya kuanzisha harakati za kumuadhibu baada ya kuaptikana ametumia dawa za kusisimua misuli.
Marufuku hiyo ni ya mda hadi pale uamuzi wa mwisho utakapoafikiwa na kitengo cha maadili cha shirikisho hilo.
Sakho mwenye umri wa miaka 26 alipatikana ametumia dawa za kusisimua misuli kufuatia ushindi wa mechi ya taji la Europa dhidi ya Manchester United mnamo tarehe 27 mwezi Machi.
Aliamua kutopinga matokeo hayo.Tarehe ya kutolewa kwa adhabu kamili itatangazwa baadaye.
Raia huyo wa Ufaransa na kilabu yake walikubaliana kwamba hatoshiriki katika mechi yoyote hadi pale Uefa itakapokamilisha uchunguzi wake
No comments
+255716829257