Habari mpya

Mvua kubwa: Mafuriko Tanzania na Kenya

Image captionMadhara ya mvua kubwa mjini Dar es Salaam
Leo imekuwa siku ngumu sana kwa uchukuzi mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Kisa na maana,,,,mafuriko.
Image captionWenyeji walitatazikika kuendesha shughuli zao za kawaida
Baadhi ya barabara kuu za kitovu hicho cha kibiashara cha Tanzania, zilikuwa hazipitiki.
Image captionMaji kila mahali
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hivi sasa kanda yote ya Afrika Mashariki imesababisha mafuriko makubwa ambayo muundo msingi wa barabara za miji ya Nairobi na Dar es Salaam haziwezi kumudu.
Magari ambayo yalijaribu kutumia mabarabara ya Dar es Salaam yalikwama mengine huku yale yenye kimo cha juu yakifaulu kupita.
Image captionMagari mengi yamekwama barabarani
Wenyeji sasa wameanza kuhoji uwezo wa muundo msingi wa maji taka wa mji huo wa Dar es Salaam hususan ukizingatia kuwa ndio sasa msimu wa mvua umeanza.
Mtangazaji wetu wa Dar es Salaam Sammy Awami amefaulu kuondoka nyumbani kwake na katika pita pita zake ametutumia picha hizi zinazoonesha hali halisia ya baadhi ya mabarabara ya Dar es Salaam.
Image captionWenye magari mjini Nairobi wataabika mabarabarani
Nchini Kenya hali sio tofauti.
Barabara ya kisasa ya Thika Super Highway haipitiki baada ya mvuo kubwa kunyesha mchana na kusababisha mafuriko makubwa.
Image captionMtabiri wa hali ya hewa anasema mvua bado inatarajiwa
Kinaya ni kuwa mtabiri wa hali ya hewa anasema kuwa mvua kubwa inatarajiwa kunyesa mjini Nairobi na maeneo mengi ya nchi.
Wenyeji wa mji huo wa Nairobi wameanza kutoa hasira zao kwenye mitandao ya kijamii wengi wakipiga picha maeneo yaliyokumbwa na mafuriko.
CHANZO: BBC

No comments

+255716829257