.
Katika miaka ya hivi karibuni, suala la upara ( baldness ) linatajwa kuwasumbua vijana wengi wa kiume. Miaka ya tisini kurudi chini ilikuwa ni aghalabu sana kumuona kijana wa miaka 25 akiwa na upara, na mara nyingi suala la upara lilikuwa likihusishwa na uzee,lakini leo hii hali ni tofauti sana, kwani kuna idadi kubwa sana ya vijana wa kiume wenye umri wa kuanzia miaka 25 hadi 45 wana okabiliwa na tatizo la upara. Pamoja na kwamba, kutokuwa na nywele hakuwezi kukamfanya mwanadamu akashindwa kuishi, lakini katika dunia ya sasa ya mitindo na utandawazi kuwa na upara ni jambo linalo wapa shida sana wahusika. “
KIPARA HUSABABISHWA NA NINI ?
Yapo mambo mengi sana ambayo ndio chanzo cha watu kuwa na upara . Baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo :
i. Kurithi kutoka kwa wazazi ( Sababu za kijenetiki )
ii. Lishe mbovu
iii. Ukosefu wa Vitamin B6
iv. Kuwa na stress, mfadhaiko na mshuko wa moyo kwa muda mrefu
NINI TIBA YA TATIZO LA KIPARA:
Kama unasumbuliwa na tatizo la kipara, jaribu tiba hii, inawaweza kuwasaidia kama ilivyo wasaidia watu wengine.
i. Indian gooseberry oil: Mafuta haya hutayarishwa kwa kuyachemsha kwenye mafuta ya nazi. Yanasaidia sana katika kuzifanya nywele zikue vizuri. Vilevile mafuta haya yanaweza kuchanganywa na juisi ya ndimu na kasha kuyatumia kama shampoo, ukifanya hivi itasaidia katika kuchochea ukuaji wa nywele na kuzuia kukatika kwa nywele.
Margosa: Majani ya Margosa yana faida kubwa sana kwa mtu anaye taka kujitibu tatizo la upara. Mafuta haya yanaua chawa na vijidudu wengineo na kuzifanya nywele kuwa ndefu.
Tui la Nazi : Fanya masaji ya kichwani kwa kutumia tui la nazi. ( Masaji hii ifanyike katika sehemu yenye kipara )
Kitunguu Maji : Kata kitunguu maji, kichovye kwenye asali na ukitumie kujisugua kwenye sehemu iliyo athirika. Fanya hivyo mara tatu kwa siku.

No comments
+255716829257