Habari mpya

Muhtasari: Habari kuu leo Ijumaa

1. Kenyatta ataka hatua madhubuti kulinda ndovu

Kenya
Image captionKenya inajiandaa kuteketeza shehena kubwa ya pembe Jumamosi
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa wito wa hatua madhubuti kuchukuliwa dhidi ya biashara haramu ya pembe, kabla ya kongamano la viongozi wa bara Afrika la kujadili mikakati ya kuwalinda ndovu.
Rais Kenyatta amesema kuwa ndovu wanakabiliwa na hatari ya kuangamizwa na kizazi kipya cha wawindaji haramu, waliojihami vilivo na walio na uhusiano wa kimataifa, na matokeo yake yamekuwa mabaya sana.

2. UK yashauriana na Cuba

CubaImage copyrightReuters
Image captionNdiyo ziara ya kwanza ya waziri wa mambo ya nje wa Uiongereza Cuba tangu 1959
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Philip Hammond ameshiriki kikao cha mzungumzo na mwenzake wa Cuba Bruno Rodríguez, katika ziara ya kwanza tangu mapinduzi ya mwaka 1959. Mazungumzo hayo yalijikita katika vigezo vinne muhimu: huduma za kifedha, kawi, elimu ya juu na utamaduni.

3. Watu 50 wauawa katika mashambulio Aleppo

BasharImage copyrightAP
Image captionSerikali ya Rais Bashar al-Assad imeshutumiwa kwa kutositisha vita
Maafisa wa ulinzi wa raia katika mji mkuu wa Syria Aleppo, wanasema kuwa karibu watu 50 waliuwawa baada ya mashambulio ya angani yaliyotekelezwa na vikosi vya serikali, katika hospitali moja Jumatano usiku.
Wafanyikazi hao, wa kundi linalojulikana kama "White Helmets" walikuwa wakichimba vifusi saa 24 baada ya mashambulizi hayo ya mabomu.

4. Biden afanya ziara ya ghafla Iraq

IraqImage copyright
Image captionMaandamano yalifanyikwa wiki hii kupinga serikali ya Iraq
Makamu wa rais wa Marekani, Joe Biden, ameiunga mkono serikali ya Iraq iliyoko taabani, baada ya ziara yake ya ghafla, na ya kwanza nchini humo kwa kipindi cha miaka mitano.
Ikulu ya White House inasema ziara hiyo ilikuwa ishara ya kuunga mkono serikali ya Iraq, kutokana na juhudi za waziri mkuu Haider al-Abadi.

5. Iran yaitaka Marekani kuachilia mali

MarekaniImage copyright.
Image captionMarekani inazuilia mali ya takriban dola bilioni mbili
Iran imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuihimiza Marekani, kuachilia mali yake yaliyoshikiliwa katika benki za Marekani, sambamba na makubaliano ya mwaka uliopita ya vikiwazo wa kinyuklia.
Iran imeghadhabishwa na uamuzi wa mahakama ya juu nchini Marekani kuwa mali yake yote, yenye thamani ya dola bilioni mbili, iliyoshikiliwa nchini Marekani, ni lazima ikabidhiwe jamaa za watu waliouwawa na makundi yanayohusishwa na Tehran.

7. Maafisa 20 wajeruhiwa katika maandamano Ufaransa

LyonsImage copyrightAFP
Image captionMaandamano yalifanyika katika miji mingi
Zaidi ya maafisa 20 wamejeruhiwa nchini Ufaransa katika makabiliano kati yao na waandamanaji wanaopinga marekebisho ya leba.
Machafuko mabaya zaidi yalishuhudiwa mjini Paris.
Makabiliano hayo aidha yalishuhudiwa katika miji ya Nantes, Lyon, Marseille na Toulouse.
Waziri mkuu wa Manuel Valls alilaani machafuko hayo, na kuwalaumu "wachache wasiowajibika".

8. Spika wa zamani amshutumu Cruz

CruzImage copyrightAP
Image captionBoehner amesema hawezi kumuunga mkono Cruz
Aliyekuwa spika wa bunge la wawakilishi nchini marekani John Boehner amemtaja mwaniaji wa urais wa marekani kwa tiketi ya chama cha Republican Ted Cruz, kuwa shetani binadamu. Bw Boehner, ambaye ni mwanachama wa Republican, amesema kuwa kamwe hatamuunga mkono Ted Cruz iwapo atateuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kuwania urais.

9. Colombia yahalalisha ndoa za jinsia moja

ColombiaImage copyrightAFP
Image captionNdilo taifa la nne kuhalalisha ndoa hizo Amerika Kusini
Mahakama ya juu zaidi nchini Colombia imehalalisha rasmi ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Hatua hiyo inaifanya Colombia kuwa taifa la nne kuhalalisha ndoa hizo katika mataifa ya Kilatino, Amerika Kusini.

10. Sarafu za Kirumi zapatikana Uhispania

SevilleImage copyrightAFP
Image captionSarafu hizo zimepatikana karibu na mji wa Seville
Wafanyikazi wa ujenzi kusini mwa Uhispania wamegundua akiba kubwa ya sarafu za kale za Kirumi, wakati wakifanya ukarabati kwenye mabomba ya maji.
Maelfu ya sarafu hizo za shaba, zilizo na uzani wa kilo mia 6, zilipatikana zikiwa zimefichwa kwenye makopo katika mji wa Tomares karibu na Seville.

No comments

+255716829257