Habari mpya

Polisi wamzuia Besigye kukutana na maafisa wa FDC

Image copyrightAP
Image captionPolisi wamzuia Besigye kukutana na maafisa wa FDC
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye anapanga kufanya mkutano na wanahabari nyumbani kwake anakotumikia kifungo cha nyumbani.
Besigye ambaye amepinga uhalali wa matokeo ya uchaguzi alikuwa anapanga kukata rufaa lakini amezuiliwa nyumbani kwake hadi leo siku ya mwisho kikatiba anayoruhusiwa kukata rufaa.
Bwana Besigye anadai uchaguzi haukuwa wa huru na wa haki.
Serikali ya Yoweri Museveni, inasema inamshikilia kiongozi huyo wa upinzani ilikumzuia kuzua rabsha ama kuwachochea wafuasi wake kuzusha ghasia nchini Uganda kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliokamilika majuma mawili yaliyopita.
Rais Yoweri Museveni ambaye ameiongoza Uganda kwa miaka 30 sasa alishinda hatamu nyengine na asilimia 60 % ya kura za urais.
Besigye alimaza katika nafasi ya pili.
Image captionMwenyekiti wa chama cha FDC meja jenerali Mugisha Muntu
Awali kulikuwa na kizaza maafisa wa polisi na jeshi la kupambana na ghasia walipowakamata wandishi wa habari aliokuwa wakiripotia nje ya nyumba ya kiongozi huyo wa chama cha FDC.
Vilevile viongozi wa chama hicho wakiongozwa na mwenyekiti Meja Jenerali Mugisha Muntu waliwafahamisha waandoishi kuwa watajaribu kumfikia kiongozi wao fauka ya kifungo chake cha nyumbani ambacho walidai si halali.
Besigye alikamatwa siku moja baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa nje ya afisi za chama chake.
Meja jenerali Muntu amefutilia mbali pendekezo la polisi kuwa watumiwe kama wapatanishi kati yao na Besigye.
''Wamependekeza eti tusimame nje tuwatume wazungumze naye kisha waje watupashe aliyoyasema ,,,kwa kweli hii ndio kiwangoupuzi wa kidikteta tunaostahimili '

No comments

+255716829257