Habari mpya

Benki ya Barclays kuuza biashara zake Afrika

BiasharaImage copyrightReuters
Image captionBaadhi ya matawi ya Barclays Afrika yamekuwa yakitatizika kibiashara
Benki ya Barclays imetangaza kwamba inapanga kuuza biashara zake barani Afrika, baada ya kuhudumu kwa karne moja barani.
Benki hiyo, wakati wa kutangaza matokeo ya kifedha ya mwaka 2015, imesema inapanga kuuza asilimia 62.3 ya biashara zake Afrika katika kipindi cha miaka miwili hadi mitatu ijayo.
Imesema uamuzi huo ulikuwa mgumu sana kuufanya ikizingatiwa kwamba nembo ya benki hiyo katika baadhi ya mataifa ya ni thabiti sana.
Barclays imesema faida yake ya kila mwaka ilishuka asilimia 2 hadi £5.4bn mwaka wa kifedha wa 2015.
Aidha, benki hiyo itapunguza mgawo wake wa faida kwa kila hisa kwa zaidi ya nusu hadi 3p mwaka 2016 na mwaka 2017.
Benki hiyo imepunguza pesa inazotenga kama bonsai kwa wafanyakazi wake kwa mwaka 2015 kwa asilimia 10 hadi £1.67bn.
Barclays imesema inapanga kurahisisha biashara zake na kuangazia vitengo viwili vikuu, Barclays UK na Barclays Corporate & International.
BarclaysImage copyrightGetty
Image captionBarclays itauza biashara zake katika kipindi cha hadi miaka mitatu
"Barclays kimsingi inafuata njia iliyo sahihi, na katika uhalisia wake, ukiangalia kitovu chake, ni biashara inayofanya vyema sana,” amesema afisa mkuu mtendaji wa benki hiyo Jes Staley taarifa yake kwenye ripoti matokeo ya kifedha ya benki hiyo.
"Lakini bila shaka kuna mambo mengi tunayohitaji kufanya na maeneo ambayo tunaamini tunaweza kuchukua hatua haraka na kuhakikisha Barclays inafanya vyema sana kama inavyotakikana.”
Awali, meneja mkurugenzi wa Benki ya Barclays nchini Kenya Jeremy Awori alikuwa ametoa wito kwa wateja wa benki hiyo kutokuwa na wasiwasi.
"Akaunti zenu za benki ziko salama na hazitaathirika kwa vyovyote vile. Nawahakikishia kwamba pesa zenu ziko salama," alisema Bw Awori kupitia taarifa.

No comments

+255716829257