Habari mpya

Korea Kaskazini yatangaza kamanda mpya wa jesh

Image captionAliyekuwa mkuu wa majeshi Ri Yong-gil, alinyongwa baada ya kutuhumiwa kuhusika na ufisadi
Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vimethibitisha kuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un amemchagua mkuu mpya wa majeshi.
Aliyekuwa mkuu wa majeshi Ri Yong-gil, alinyongwa baada ya kutuhumiwa kuhusika na ufisadi pamoja na kuunda chama mbadala cha upinzani.
Pyongyang haijasema lolote kuhusiana na madai hayo , lakini mapema leo Jumapili runinga inayomilikiwa na serikali imetangaza kjina la mkuu mpya wa majeshi.
Image captionKorea Kaskazini yatangaza kamanda mpya wa jeshi
Ri Myong-su, sasa ndiye kamanda anayesimamia jeshi.
Duru kutoka Korea Kusini wanasema mabadiliko hayo yanathibitisha kuwa makumi ya maafisa wakuu jeshini wameuawa Korea Kaskazini tangu Kim Jong-un atwae madaraka mwaka wa 2011.

No comments

+255716829257