Habari mpya

Hatimaye Australia yamhurumia mtoto Asha

Image copyrightReuters
Image captionHatimaye Australia yamhurumia mtoto Asha
Serikali ya Australia imetangaza kuwa mtoto aliyezaliwa na wahamiaji nchini humo na ambaye alikuwa akitibiwa majeraha ya moto katika hospitali ya Brisbane atakubaliwa kusalia nchini humo.
  • Madaktari wamekataa kumruhusu Asha , mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja, aondoke hospitalini kwa sababu anakabiliwa na tishio la kurejeshwa baharini katika kambi wanakowazuilia wahamiaji na wakimbizi katika kisiwa cha Nauru kilichoko katika bahari ya Pacific.
Waziri wa uhamiaji, Peter Dutton, amesema kuwa sasa mtoto huyo na mamake wataruhusiwa kujiunga na jamii nchini Australia na wala hawatazuiliwa katika kambi hiyo.
Lakini akasisitiza kuwa watarejeshwa katika taifa walikotoka iwapo maombi yao ya uhamiaji nchini Australia itakataliwa.
Image copyrightREUTERS
Image captionMadaktari wamekataa kumruhusu Asha , mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja, aondoke hospitalini kwa sababu anakabiliwa na tishio la kurejeshwa baharini
Sera za Australia ya kuwafungia wahamiaji katika visiwa vya Nauru na Papua New Guinea vimekashifiwa na wapiganiaji wa haki za kibinadamu wanaodai kuwa nchini hiyo inatelekeza wajibu wake wa kimataifa kuwalinda na kuwapa makao wakimbizi wanaofika katika mipaka yake.

No comments

+255716829257