Cameron aomba kuungwa mkono kusalia Ulaya
Waziri Mkuu wa Uingereza , David Cameron, ameiambia BBC, kwamba Uingereza itakuwa na nguvu zaidi katika ulimwengu, ikibaki katika Umoja wa Ulaya iliofanyiwa mabadiliko.
Alisema hayo siku moja baada ya kutangaza, kuwa kura ya maoni itafanywa mwezi Juni, kuamua kama Uingereza ibaki au itokea katika umoja huo wa ulaya.
Cameron, amewaomba wabunge wa chama chake waunge mkono kusalia ndani ya muungano huo.
Meya wa mji wa London, Boris Johnson, tayari ameonesha dalili za kuunga mkono kuondoka kwenye muungano wa ulaya.
Cameron anasema alifikiwa makubaliano na nchi nyengine za Umoja wa Ulaya kuhusu mabadiliko, ambayo wadadisi walisema hayatowezekana kuyapata.
Lakini kiongozi wa chama cha UKIP, kinachotaka kujitoa katika umoja wa ulaya, Nigel Farage, alisema mabadiliko hayo hayakufanikiwa kushughulikia maswala kama uhamiaji
Farage anasema Cameron alishindwa kuwashawishi wenzake kutatua maswala makubwa kama uhamiaji.
Waziri kiongozi wa Scotland, Nicola Sturgeon, alisema marekibisho aliyopata Bwana Cameron, hayakuwa makubwa.
No comments
+255716829257