WADAU WA MAZINGIRA WAOMBA KIPAUMBELE KUTOKA KWA SERIKALI.
Na Gidion Ramadhani
Arusha.Wadau mbalimbali wanaojishughulisha na utunzaji wa
mazingira jijini Arusha wameelezea changamoto mbalimbali wanazozipata katika
shughuli hizo ikiwa ni pamoja na kukosa kipaumbele kutoka katika serikali na
jamii kwa ujumla.
Walisema hayo wakati walipokua wakizungumza na gazeti hili
lilipotembelea eneo wanapofanyia shughuli zao
lililopo Mianzini, jijini Arusha ambako walitaja baadhi ya shughuli
wanazozifanya kuwa ni pamoja na uoteshaji wa bustani za miti na maua ambayo
huuzwa kwa watu mbalimbali wakiwepo wageni na wenyeji ambayo kwa namna moja
husaidia utunzaji wa mwzingira.
“Tunatengeneza
bustani kubwa za miti na maua ya aina mbalimbali ambayo tunawauzia watu kutoka
sehemu mbalimbali wakiwemo wenyeji na wageni ikizingatiwa kuwa Arusha ni jiji
la kitalii hivyo wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi huitembelea Arusha na
kujionea shughuli tunazofanya na asilimia kubwa kuvutiwa nazo” alisema Bi Maria
Emmanuel mmoja wa wadau hao.
Wadau hao walizitaja changamoto mbalimbali wanazokumbana
nazokumbana nazo kuwa ni kukosa maeneo maalum ya kufanyia shughuli zao amoja na
jamii kutotambua mchango wao katika utunzaji wa mazingira..
“Tatizo kubwa ni
kwamba hatuna maeneo maalum tuliyotengewa na serikali kwa ajili ya kufanyia
shughuli zetu,tunajikuta tukifanyia pembezoni mwa barabara ambako mara nyingi
tunapata misukosuko mingi kutoka kwa wakala wa ujenzi wa barabara(TAN ROAD)
hata hivyo jamii inayotuzunguka pia inashindwa kutambua tunachofanya wakati
mwingine bustani zetu huvurugwa na mmianzini.
Wameiomba serikali,mashirika yanayojihusisha na utunzaji wa
mazingira pamoja na wanajamii wote wenye mapenzi mema na wenye urafiki na
mazingira kuwaunga mkono wadau hao ikiwemo kupatiwa maeneo maalum ya kufanyia
shughuli zao pamoja na kutolewa elimu ya kutosha kwa jamii nzima juu ya
utunzaji wa mazingira na faida zake kwani mazingira bora ndio chanzo cha hali
ya hewa nzuri na upatikanaji wa mvua za kutosha.
No comments
+255716829257