VYOMBO VYA HABARI ENDELEENI KUHABARISHA NA KUFICHUA MAOVU.
Gidion Ramadhani.
Nimatumaini yangu kuwa sote tumeuanza vyema mwaka
2015,shukrani na utukufu vinastahili kuelekezwa kwa mwenyezi mungu muumba wa
mbingu na ardhi na vyote vilivyomo mwenye kuneemesha neema kubwa na ndogo,hakika
yeye ndie mwenye mamlaka pekee yakutuweka hai mpaka tumeushudia mwaka mpya.
Naamini sote tumeshudia kazi kubwa iliyofanywa na vyombo vya
habari tangu mwaka jana 2014 ikiwa ni pamoja na
kuibua,kuelimisha,kuhabarisha,kuburudisha pamoja na kuchambua masuala
mbalimbali ya kisiasa,kiuchumi na kijamii ndani na nje ya nchi yetu.
Tumeshuhudia vyombo
vya habari vikisimama kidete kutetea unyanyasaji wa watoto mfano mzuri ni kwa
Yule aliyeitwa “mototo wa box” ambapo wasamaria wema wenye uchungu na mapenzi
ya dhati kwa watoto wanaonyanyasika walipolisikia hilo kupitia vyombo vya
habari walijikuta wakilaani vikali vitendo kama hivyo na pia sheria ikafwata
mkondo wake kwa wahusika ili iwe funzo kwa wote wenye kuwatendea vibaya watoto.
Miongoni mwa majanga yaliyotikisa nchi ni pamoja na mlipuko
wa ugonjwa hatari wa Dengue ambao ungeweza kusababisha maafa makubwa nchini
lakini kupitia kampeni kubwa iliyofanywa na vyombo vya habari ili kuhamasisha
na kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo
hatimaye kwa Baraka za mungu ugonjwa ukatoweka.
Sanjari na hayo nchi za Afrika magharibi, Sierra
leon,Nigeria,Guinea,Senegal na nchi ya jirani,Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
zilijikuta zikigubikwa na wimbi la ugonjwa hatari wa Ebola ambapo mamilioni ya
watu walifariki dunia kutokana na ugonjwa huo lakini vyombo vya habari vya
ndani na nje vilipambana nab ado vinapambana kikamilifu kuhakikisha vinasambaza
habari katika nchi hizo na kote duniani kuwatahadharisha watu juu ya ugonjwa
huo na pia kuhamasisha mashirika mbalimbali ya kibinadamu duniani kutoa misaada
mbali mbali kwa waathirika ikiwemo kinga,dawa pamoja madaktari bingwa ili
kuutokomeza kabisa ugonjwa wa Ebola.
Hata hivyo vyombo vya habari havikuishia hapo hata katika
kinyang`anyiro cha miss Tanzania mwaka 2014,ilikua watanzania wapigwe changa la
macho lakini vyombo vya habari vilikua macho na kuweka mambo hadharani juu ya
udanganyifu wa Bibie Sitti Mtemvu na hatimaye kuvuliwa taji hilo na kuvishwa
mwenye vigezo vinavyokubalika.
Tugusie sakata zito la akaunti ya Escrow ambapo almanusra
watanzania wapoteze mabilioni ya fedha ya kodi zao pasipo kujijua,zaidi ya
billion 300 ziligundulika kuchukuliwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi
ikiwa umati wa watanzania,wakubwa kwa wadogo,wakike na wakiume wakiendelea
kutaabika katika mateso ya kukosa huduma muhimu za kijamii kama vile hospitali
bora hakuna madaktari wanagoma huku dawa hakuna,maji safi na salama bado ni
tatizo sugu wakina mama na watoto vijijini hufwata maji kilometa tatu mpaka tano,elimu
bora ni bado tatizo shule hazina madawati,vitabu wala maabara,hakuna nyumba za
waalimu na bado wanalipwa mishahara midogo.
Vyombo vya habari vililiona hilo na
kulifwatilia kwa ukaribu kule bungeni na kutoa taarifa kwa umma hatimaye
wahusika kubainika na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Tukiangazia halihalisi ya mwaka huu 2015 yapo mambo mengi yanayokuja mbele yetu
ikiwemo mchakato wa katiba mpya ambapo wananchi hutarajiwa kutoa maoni yao,
nina imani kuwa vyombo vya habari vitaonesha ushirikiano wa hali ya juu katika
suala hili kama ilivyokua mwaka jana wakati wa kutoa maoni juu ya rasimu ya
katiba mpya ambapo wananchi walikua makini sana kusikiliza redio,kutizama runinga,kusoma
magazeti pamoja na kuperuzi mitandao mbalimbali ya kijamii ili kujua kinachoendelea
juu ya mchakato mzima wa katiba mpya.
Hali kadhalika lipo suala jingine nyeti ndani ya huu mwaka
ambalo ni uchaguzi mkuu wa rais,wabunge na madiwani,ni matumaini yangu kuwa
kila mtanzania anayo shauku kubwa yakutaka kujua uchaguzi utakuaje na pia
naamini vyombo vyetu vya habari vitakua mstari wa mbele kutuhabarisha kila
linalojiri katika tukio hili zima la kidemokrasia kuanzia kipindi cha kampeni
mpaka uchaguzi.Tutapata kuziskia hoja na sera mbalimbali za wagombea wetu
kupitia vyombo vya habari sanjari na kufichuliwa kwa maovu yote
yatakayojitokeza kinyume na sheria na utaratibu wa uchaguzi.
Kwa pamoja tumuombe mungu atuongoze tuweze kupata katiba
bora yenye kusimamia haki nausawa kwa watu wote na yenye kuleta chachu ya
maendeleo katika taifa hili lililojaliwa kila aina ya utajiri zikiwemo mbuga za
wanyama,milima mirefu,mito,bahari na maziwa,misitu mikubwa na ardhi yenye
rutuba,migodi mikubwa ya madini adimu duniani,nishati ya gesi pamoja na watu
wenye busara,ukarimu na upendo wa hali ya juu pia tumuombe mungu atujalie
uchaguzi huru na tulivu wa haki na usawa.Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki
Tanzania.Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Waziri wa Habari Michezo na Utamaduni Fenera Mkangala.
No comments
+255716829257