Habari mpya

Nick Cannon ameahidi kumalizia makala ya Nipsey kuhusu ugunduzi wa dawa ya UKIMWI uliofanywa na Dr.Sebi


Unaambiwa kuwa kuna mengi yamezungumzwa baada ya kifo cha Rapper Nipsey Hussle, ambapo malalamiko mengine yanapelekwa katika serikali ya Marekani na kuihusisha kwenye mauaji hayo yaliotokea March 31,2019 mjini Los Angeles Marekani.

Inaelezwa kuwa wengi wanaamini Rapper Nipsey ameuawa kutokana na harakati zake za kutaka kuiachia makala(documentary) ambayo inaelezea kuwa kuna tiba ya dawa ya virusi vya UKIMWI  pamoja na Saratani ambapo dawa hiyo iligunduliwa na Marehemu Dr. Sebi aliyefariki August 06,2016.

Inaripotiwa kuwa endapo documentary hiyo ingeachiwa basi dawa ya UKIMWI ingejulikana na kungepelekea serikali ya Marekani kukosa fedha ambazo tayari imekuwa ikiingiza kwa kutengeneza kinga pamoja na dawa za kupunguza makali. 
Mwimbaji na muigizaji Nick Cannon ameutumia ukurasa wake wa Instagram kusema kuwa ataendelea kuyaenzi mambo ambayo Nipsey ameyaacha ikiwemo la kuiachia documentary ya Dr. Sebi na kusisitiza kuwa hawawezi kuwaua wote na ataimailizia na kuiachia documentary hiyo.

No comments

+255716829257