DMX apewa shavu kwenye filamu ya ‘Chronicle of a serial killer’
Rapper DMX apata dili ikiwa ni miezi kadhaa imepita toka amalize kifungo chake, DMXanatajwa kurejea kwenye filamu yake ya kwanza iitwayo ‘Chronicle Of A Serial Killer’iliyopo chini ya muongozaji Steve Stanulis.
Kwa mujibu wa mtandao wa Hot New Hip Hop umeripoti kuwa rapper huyo ndio muigizaji mkuu (main character) ambapo uhusika aliopewa DMX ndani ya filamu hiyo ni kuwa kiongozi wa upelelezi (detective) ambapo utengenezaji utaanza mwezi June mwaka huu jijini New York.
“Sina mashaka na DMX ataleta kitu cha tofauti kwenye nafasi yake ya uigizaji, nina furaha kuwa miongoni mwa waigizaji wenye vipaji kwenye hii filamu, nina matumaini ya kufanya nae kazi pamoja na watu wengine kwenye kipindi hiki” >>> Steve Stanulis
No comments
+255716829257