Habari mpya

Yanga wafunguka baada ya mchezaji wao kufungiwa miezi 14

Shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kwa afisa habari wake Clifford Ndimbo limetangaza kufungiwa miezi 14 kucheza soka kwa mchezaji wa Yanga SC Mohammed Issa ‘MO Banka’ kutokana na kuthibitika kuwa ametumia dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya Bangi.
Banka baada ya uchunguzi wa maabara kufanywa na kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni ya kanda ya tano RADO, Banka amegundulika kuwa alitumiwa dawa za kulevya aina ya Bangi.

Banka amefungiwa miezi 14 kuanzia December 14 2017 na atamaliza adhabu yake February  8 2019, afisa habari wa Yanga Dismas Ten ameongea na waandishi wa habari baada ya kutoka kwa taarifa hizo “Taarifa imetoka leo nadhani tutakuwa na tamko lingine baada ya kupokea barua kutoka TFF, kwa sababu ni lazima kuchukua barua ili uchukue hatua zingine” Alisema Ten

No comments

+255716829257