Habari mpya

Waziri wa ulinzi wa Israel ajiuzulu


Waziri wa ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman alitangaza kujiuzulu kutoka kwa wadhifa wake siku ya Jumatano  na kutoa wito wa uchaguzi wa mapema kufuatia kutokukubaliana kuhusu mkataba wa kusitisha mapigano, na kusababisha serikali kuingia katika mzozo. 

Lieberman alitangaza uamuzi wake huo mbele ya waandishi wa habari na kueleza sababu ya kufikia hatua hiyo na kuongeza kwa kusema kuwa kunatakiwa makubaliano ya tarehe ya uchaguzi mapema iwezekanavyo na pia kwamba chama chake kitajiondoa kwenye serikali ya muungano ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu na kumuacha waziri mkuu huyo akiwa na wingi wa kiti kimoja tu bungeni.

Alikosoa uamuzi wa serikali kukubaliana kusimamisha mashambulizi ya angani siku mbili katika Gaza ili kuzuia mfululizo wa mashambulizi ya makombora kutoka Gaza kusini mwa Israeli, badala ya kuzindua vita kikamilifu dhidi ya Gaza.

No comments

+255716829257