Habari mpya

Ugonjwa wa koo wamuweka Tekno nje ya muziki


Manager wa mwimbaji Tekno Miles kutokea NigeriaUbi Franklin ametoa taarifa kuhusiana na ukimya wa Mwimbaji huyo huku akitaja sababu kuwa ni kuharibika kwa koo la sauti na hivyo Tekno anapaswa kukaa nje ya kazi ya Muziki.
Ubi Franklin ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuwa madaktari wameshauri Mwimbaji huyo akae nje ya maisha ya Muziki ili apatiwe matibabu hii ni baada ya kubaini tatizo linalomsumbua.
Ubi Franklin ametaja sababu iliyofanya kupelekea kwa kuharibika koo la sauti na kusema kuwa imetokana na kuimba bila kupata mapumziko  ya muda mrefu kwahiyo kutokana na hali yake Tekno hatoweza kuimba wala kufanya shows ila ataachia baadhi ya ngoma zake ambazo ziko tayari.











Hii sio mara ya kwanza kwa mwimbaji Tekno kuaa nje ya muziki,Mwezi wa April 2017Tekno alitangaza kuahirisha baadhi ya shows zake na kwenda nchini Marekani kwaajili ya matibabu baada ya kusumbuliwa na ongezeko la acid mwilini na mara nyingine mwili wake ulikuwa ukikosa nguvu na hivyo kuombwa kupumzika na masuala ya muziki.


No comments

+255716829257