Habari mpya

Fellaini kaipeleka Man United 16 bora Champions League


Michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 inazidi kupamba moto kwa timu mbalimbali kuonesha dhamira ya kutoka hatua ya Makundi na kuingia hatua ya mtoano ya 16, michezo nane imechezwa usiku wa November 27 na tumeshuhudia baadhi ya timu zikiingia hatua ya 16 bora zikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Man United ni miongoni mwa timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya 16 bora baada ya ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Fellaini dakika za majeruhi wakati club za FC Bayern Munich, Juventus, Real Madrid, AS Roma na Man City zote zikifuzu 16 bora zikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Ushindi wa goli 1-0 wa Juventus dhidi ya Valencia unamfanya Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanza kufanikiwa kupata ushindi katika jumla ya michezo 100 ya UEFA Champions League akiwa na timu mbalimbali zikiwemo Real Madrid na Juventus.

No comments

+255716829257