Habari mpya

Mchezo mpya wa bahati nasibu "Supa Tano" wazinduliwa

Kampuni ya maarufu inayochezesha michezo mbalimbali ya bahati nasibu The Network  Novemba 14 2018 wamezindua mchezo mpya wa bahati nasibu uitwao supa tano ambapo washindi mbalimbali wataweza kujishindia mamilioni ndani ya dakika 10 tu  kwa kiwango kuanzia shilingi elfu moja hadi elfu ishirini.
Mchezo huu ndio utakuwa wa kwanza nchini Tanzania ambapo mshindi anaweza kujishindia kiasi kikubwa ndani ya dakika kumi na vie vile ndio utakuwa unatoa fursa nyingi zaidi za ushindi hapa nchini.
Meneja wa fedha wa The Network Jacob Milinga amezungumza na waandishi wa habari kwamba kupitia supa tano mchezaji anapata nafasi nyingi zaidi za ushindi kwani kila namba anayolinganisha analipwa kuanzia namba 2,3,4 namba 5 kwenye droo za kila dakika 10 na wakati huo kila shilingi 1000 yake inampa nafasi yakuingia kwenye SupaMzuka Jackpot siku za jumapili na jumatano.
Mchezo huu wa supa tano unaendeshwa kwa uwaz na usimamizi wa serikali kupitia bodi ya michezo ya kubahatisha Tanznaia, hivyo matokeo yote ya washindi na zawadi walizoshinda yatawekwa kwenye tovuti ya www.supatano.co.tz -Jacob Milinga

No comments

+255716829257