Habari mpya

BREAKING NEWS : Mbunge wa jimbo la Temeke (CUF) ajiuzulu

PICHA:Abdallah Mtolea akitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kutangaza kujiuzulu Ubunge
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdallah Mtolea wa Chama cha CUF ametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama hicho pamoja na kuachia nafasi yake ya Ubunge kuanzia hivi sasa.

Mtolea ametangaza uamuzi huo bungeni jijini Dodoma hii leo Novemba 15, 2018 ikiwa ndio tarehe ya mwisho iliyowekwa na CCM kwa viongozi wa vyama vingine wanaotaka kuhamia CCM na kupewa dhamana ya kutetea udiwani na ubunge wao kwa tiketi ya chama.


Taarifa hizo zimethibitishwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ambaye amesema amepokea barua ya kujiuzulu kwake.

No comments

+255716829257