Habari mpya

Man United imekubali kipigo cha 52 cha Man City Nov 11 2018

Man City wakiwa nyumbani Etihad wamefanikiwa kuendeleza jitihada za kutetea taji la EPL kwa kuifunga Man United kwa magoli 3-1, magoli ya Man City yamefungwa na David Silva dakika ya 11, Sergio Aguero dakika ya 48 na Gundogan dakika ya 86 wakati goli pekee la kufutia machozi la Man United lilifungwa na Anthony Martial kwa penati dakika ya 58.
Baada ya kupoteza game hii Man United dhidi ya Man City anakuwa amefungwa mara 52 toka walipokutana kwa mara ya kwanza October 3 1891 katika mchezo wa FA, kipindi hicho Man City ikiitwa Ardwick, timu hizo zimekutana jumla mara 177, Man United akishinda mara 73 na sare mara 52, Man United sasa wapo nafasi ya 8 wana point 20 na Man City wapo nafasi ya kwanza wana point 32.

No comments

+255716829257