Habari mpya

Aslay afunguka haya baada ya kudondoka stejini nchini Kenya

Staa wa Bongo Fleva  Aslay amepata ajali alipokuwa akitumbuiza jukwaani Kisumunchini Kenya na kusema kuwa kuanguka kwake hakukufanya aache kuburudisha mashabiki wake nchini humo.
Aslay alitumia ukurasa wake wa instagram kuelezea tukio na kusisitiza kwa kusema kuwa ni jambo la kawaida kwa wasanii kupata changamoto wakiwa juu ya stage na kuamini kuwa kuanguka kwake ni moja ya changamoto.
“Ni Kawaida kwa Wasanii kupatana na changamoto jukwani, na Jana ilikuwa zamu yangu, yalitokea Haya punde tu nilipopanda jukwani kwa bahati nzuri sikuumia ,nilirejea jukwani na kuburudisha Mashabiki wangu wa Kisumu waliyojitokeza kwa wingi. Asanteni sana nyote Mwenyezi Mungu Awabariki!!!”


No comments

+255716829257