Habari mpya

Huu ndio Msimamo wa TPL, Simba SC waichapa Alliance

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya Simba SC baada ya ushindi dhidi ya Stand United  wameingia tena uwanjani kupambana dhidi ya Alliance FC ya Mwanza katika muendelezo wa game zake za Ligi Kuu.
Simba wakiwa uwanja wa Taifa DSM wamefanikiwa kupata ushindi mnono wa magoli 5-1, magoli ya Simba yakifungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 10 na 62, Asante Kwasidakika ya 30, Adam Salamba dakika ya 70 na Clotous Chama dakika ya 86, wakati goli pekee la Alliance lilifungwa na Khamis dakika za nyongeza.
Ushindi huo saa umeifanya Simba SC kuwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara inayoshirikisha jumla ya timu 20, kwani Simba ina point 20, Ligi ikiongozwa na Azam FC ambao wana point 24 kwa upande wa Alliance FC wao wapo nafasi ya mwisho kwa kuwa na point sita wakicheza game 11.

No comments

+255716829257