Habari mpya

WizKid apiga shavu Nike

Jina la Wizkid ‘Starboy’ linazidi kuvuka mipaka na hii ni baada ya kuungana na kampuni ya Nike na kufanya nayo biashara ya jezi “Nike by Wizkid” na kuvunja rekodi kutokana na toleo la kwanza la jezi hizo kuisha ndani ya dk 10.
Jezi hizo zenye jina la ‘Starboy’ zinauzwa kwa thamani ya laki moja na elfu 70 za Kitanzania, baada ya kuingizwa sokoni na kuuzwa katika mtandao wa Nike ziliisha ndani ya dakika 10 zikiwa ni bidhaa za kwanza kuachiwa na Nike tangu waachie kampeni ya ‘Just do it’
Kupitia ukurasa wa instagram wa Wizkid ameandika “Hiyo ilikuwa haraka zimeisha ndani ya dakika 10, nawapenda wote, Mungu anafanya kazi kwa bidii kuliko shetani”

No comments

+255716829257