Habari mpya

Waitara atangazwa kuongoza Tume ya uchunguzi ajali ya kivuko

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtangaza Jenerali Mstaafu George Waitara kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza ajali ya Mv-Nyerere na kutoa mwezi mmoja ili tume hiyo itoe majibu na  mapendekezo juu ya hatua ambazo serikali inapaswa kuzichukua.
Akizungumza na wananchi wa Ukara Waziri Mkuu amesema serikali inaendelea na hatua za awali za kuhakikisha inawachukulia hatua waliosababisha ajali hiyo na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Hatua za awali zilishachukuliwa tulishakamata wale wote ambao waliruhusu watu kujaa, na uchunguzi unaendelea, tumeunda tume iliyojaa wataalamu na vyombo vya dola ilitubaini nani hasa muhusika, tume  ina watu saba na inaongozwa na Jenerali Mstaafu George Waitara.Nimewapa mwezi mmoja ili kutoa taarifa ya tukio hilo.”

No comments

+255716829257