Habari mpya

Katika kumbukubmu ya siku yake ya kuzaliwa Ommy Dimpoz amepost picha yake akiwa ICU

Tarehe kama ya leoSeptember 13,2018  miaka kadhaa iliyopita ndio siku aliyozaliwa msanii Ommy Dimpoz ,Masnii Ali Kiba akiwa kama mtu wake wa karibu amemtakia kila la kheri katika maisha yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ali Kiba amemtaka Ommy Dimpoz akazane na aamini kuwa Mungu ana maana yake na ndie Muumbaji wa Wanyonge na Wajanja hivyo anapasa kumshukuru. 
“Happy Birthday @ommydimpoz enjoy your special day bro Na wala Usiwaze.Mwenyezi Mungu ndie Muumbaji Wa wanyonge Na wajanja . Hivyo basi tunatakiwa tumshukuru kwa kutupa/Na Kutunusuru kwasababu Mungu Ana maana yake na anatupenda Sote ..KAZA 💪🏾
#mofayabyalikiba #KingKiba”
Aidha Ommy Dimpoz, kwa mara ya kwanza amepost picha yake katika mtandao wa instagram akiwa ICU huko Afrika kusini wakati alipokuwa amefanyiwa upasuaji wa mfumo wa chakula, Unaweza kutazama kwa kubofia video hapo chini..

No comments

+255716829257