Habari mpya

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi SUMATRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRAMhandisi Dkt. John Ndunguru na kuivunja bodi hiyo kuanzia leo tarehe 24 Septemba, 2018.
Rais Magufuli amechukua hatua hiyo kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba, 2018 na matukio mbalimbali ya ajali za barabarani hapa nchini yanayosababisha vifo, ulemavu na uharibifu wa mali.
Pamoja na hatua hiyo kamati ya uchunguzi ambayo itatangazwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa baadaye leo, itaendelea na uchunguzi wa ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kama ilivyopangwa.

No comments

+255716829257