Habari mpya

Msafara wa JPM wapata ajali

Msafara wa Rais John Magufuli umepata ajali katika kijiji cha Kasuguti Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara ikihusisha magari manne kugongana na kusababisha gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari kupinduka na kupelekea baadhi ya waandishi kuumia sehemu mbalimbali za miili yao. 
Wakati ajali hiyo ikitokea, gari za Rais Magufuli zilikuwa zimepita umbali mrefu kutoka eneo ilipotokea ajali hiyo.
Taarifa za awali zinadai kwamba hali za majeruhi zinaendelea vizuri.

No comments

+255716829257