Habari mpya

EPUKA AJALI ZA BARABARANI KWA KUFANYA HAYA..

Image result for EPUKA AJALI ZA BARABARANI.
Na Ramadhani Gidion#mswahili.
Fuata Kanuni hizi za Uvukaji: 
Image result for EPUKA AJALI ZA BARABARANI.
1. Tafuta sehemu salama ya kuvuka
2. Simama kwenye ukingo wa barabara
3. Angalia magari barabarani kushoto, kulia na sehemu zote kukuzunguka, na sikiliza.
 4. Kama kuna gari linakuja liache lipite
5. Wakati hakuna gari linalokuja, vuka moja kwa moja barabara-usikimbie
6. Angalia na sikiliza magari wakati wa kuvuka Mahali salama pa kuvukia.
Chagua sehemu unapoweza kuona pande zote, na ambapo dereva anaweza kukuona. Kwa sababu hii, vuka barabara vizuri mbali na kona kali yoyote. Mahali ambapo ni salama kuvuka barabara, ni pamoja na kwenye taa za barabarani, kwenye alama za pundamilia, kiplefti, madaraja ya waendea kwa miguu na njia za chini, au mahali alipo ofi sa wa polisi, mwongoza kivuko cha shule au magari. Kuvuka kwenye kizingwa.
 Iwapo kuna kizingwa katikati ya barabara, tumia Kanuni za Uvukaji kuvuka hadi kwenye kizingwa na kisha simama. Tumia utaratibu uleule kuvuka sehemu iliyobaki ya barabara. Kuvuka kwenye alama za pundamilia. Iwapo kuna alama za pundamilia karibu zitumie. Mpe dereva muda wa kutosha kukuona na kusimama kabla ya kuvuka.
Madereva wanatakiwa kisheria wasimame pindi unapoanza kuvuka kwenye alama, lakini usivuke hadi wanaposimama. Kisha vuka moja kwa moja, lakini endelea kuangalia na kusikiliza. Kuvuka kwenye taa za barabarani. Katika baadhi ya sehemu kuna ishara za taa za barabarani zinazoyaongoza magari wakati wa kusimama na watembea kwa miguu wakati wa kuvuka. Wakati ishara ya mtu aliyewima mwenye rangi nyekundu inapoonyeshwa USIVUKE. Wakati taa zikibadilika kuonyesha ishara ya “mtu anayetembea” mwenye rangi ya kijani, angalia kuwa magari yamesimama na kisha vuka kwa uangalifu.
Baada ya muda ishara ya rangi nyekundu, au wakati mwingine ishara ya rangi ya kijani, inawaka ghafl a, na hii maana yake usianze kuvuka, kwa sababu magari karibu yataanza kwenda tena. Iwapo taa za barabarani hazina ishara maalumu kwa watembea kwa miguu, angalia kwa makini na usivuke hadi taa nyekundu zikiwaka na magari kusimama.
Pamoja na hayo, angalia magari yanayopinda kona. Kumbuka kuwa taa za barabarani zinaweza kuruhusu magari kutembea kwenye baadhi ya njia wakati njia nyingine zikiwa zimesimama. Vivuko vinavyoongozwa na polisi, askari wanaoongoza magari na waongozaji wa shule. Iwapo kuna ofi sa wa polisi au mtu mwingine mwenye mamlaka ya kuongoza magari, USIVUKE barabarani hadi wakuashirie kufanya hivyo.
Mara zote vuka mbele yao. Usipande juu ya uzio. Katika sehemu nyingine uzio umewekwa ili kuwazuia watembea kwa miguu kuvuka barabara na kuwaongoza mahali salama pa kuvukia. Usipande juu ya uzio, au kutembea katikati yake na barabara. Vuka kwenye nafasi iyowekwa. Kuvuka mitaa ya barabara moja na njia ya basi na baiskeli. Angalia ni njia ipi ambayo magari yanakwenda, kisha tumia Kanuni za Uvukaji kuvuka barabara.
 Kuwa makini sana kwa sababu magari yanaweza kuwa yanakwenda kasi sana kuliko kawaida. Usivuke katikati ya magari yaliyoegeshwa. Iwapo utalazimika kuvuka katikati ya magari, tumia ukingo wa nje wa magari iwapo barabara ina ukingo. Simama hapo na hakikisha kuwa unaweza kuona sehemu zote na kuwa madereva wenye magari wanaweza kukuona. Endelea kuvuka kwa kutumia Kanuni za Uvukaji. Usisimame mbele au nyuma ya gari lolote lililosimama ambalo injini yake haijazimwa.
Wakati wa usiku, vuka karibu na taa za mtaani. Iwapo hakuna taa za barabarani, alama za pundamilia au kizingwa ambavyo unaweza kuvitumia, vuka karibu na taa za mtaani, ili madereva waweze kukuona kwa urahisi zaidi. Vaa nguo zenye rangi inayoangaza au kung’aa ili kufanya wengine wakuone kwa urahisi wakati wa usiku. Kamwe usivuke barabara moja kwa moja nyuma au mbele ya basi. Usivuke barabara na basi  acha mpaka lipite, ili uweze kuona pande zote mbili za barabara vizuri. Usivuke mbele ya magari ya dharura.
Iwapo utayaona au kuyasikia magari ya wagonjwa, magari ya kuzima moto, ya polisi au magari mengine yoyote ya dharura yenye vimulimuli na sauti za ving’ora, usivuke barabara mpaka yapite. Kuvuka na watoto. Watoto wadogo hawajui jinsi barabara ilivyo hatari, na si wajuzi wa kuamua juu ya kasi na umbali. Kwa sababu ni watoto ni rahisi kuchanganywa, na wanaweza kufanya vitu vya hatari. Usiwaache watoto wadogo kuvuka barabara peke yao. Mara zote shika mikono yao kwa nguvu wakati wa kuvuka. Watoto hujifunza kwa mifano, kwa hiyo wakati wote tumia Kanuni za Uvukaji wakati wa kuvuka barabara, na waelezee.

Source: TAN ROAD.

No comments

+255716829257