Habari mpya

Rais Magufuli amemteua Profesa Florens Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)..

Image result for Rais Magufuli amemteua Profesa Florens Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ambapo ataanza kutumikia nafasi hiyo January 2018.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akikabidhi vyeti vya shukrani kwa wajumbe wa kamati mbalimbali  zilizohusika katika mchakato mzima wa madini Ikulu Dar es Salaam.
Image result for Prof. LuogaProf. Florens D.A.M Luoga
Rais amesema kuwa anafahamu Gavana wa sasa wa Benki Kuu, Prof. Ndulu amefanya kazi kubwa sana na kwamba takribani miezi miwili kutoka sasa atastaafu na kwamba atakayechukua nafasi yake, yupo miongoni mwa walioshiriki kwenye mchakato wa makinikia.
Akiendelea kuzungumza, Rais Magufuli alisema kuwa amemteua Prof. Luoga ambaye kitaaluma ni mwanasheria nguli katika masuala ya kodi, uwekezaji na mikataba kuchukua nafasi ya Prof. Ndulu mara atakapostaafu.
Rais aliyasema hayo alipokuwa akikosoa hatua ya BoT kutokuzuia wawekezaji wanaokuja nchini kuwekeza na badala ya kufungua akaunti ya ndani ya nchi, wanakwenda kufungua katika nchi ambazo hazitozi kodi wakati sheria ipo na inazuia hatua hiyo.
 "Leo nimeamua kumteua Gavana katika hawa nilowapa vyeti leo. Nimemteua Prof. Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu mara baada ya Gavana aliyepo kumkabidhi. Prof. Luoga ni Mtaalamu wa Taxation law,". Alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameongeza kuwa amemteua Prof. Luoga kwa sababu katika kitengo cha kodi BoT kulikuwa na matatizo lakini pia, amemteua miongoni mwa wazalendo waliopigania masuala ya madini ili kutia chachu miongoni mwa watanzania wawe wazalendo.
Prof. Luoga alikuwa miongoni mwa watanzania wanane waliofanya majadiliano na vigogo wa Barrick Gold Corporation na kuiletea manufaa mbalimbali.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI..

Wasifu wa Profesa Florens Luoga
Prof. Luoga (born in 1958) is a professional lawyer. He has a Bachelor of Laws (LL.B. Hons) from the University of Dares Salaam (1985); LL.M. from Queen's University (Canada, 1988); Master of International Law (MIL) from Lund University (Sweden, 1991); and PhD in Law from the University of Warwick (UK, 2003).

He was employed by UDSM as Tutorial Assistant in the then Faculty of Law (now University of Dares Salaam School of Law) in 1986; he then promoted to Associate Professor in 2005. He has held various administrative posts at UDSM, including the following: Chairman of the Legal Aid Committee of the then Faculty of Law (1993-1995); Associate Dean- Administration, Faculty of Law (1992-1996, 2003); Director of Undergraduate Studies (2005-2009), University Corporate Counsel and Secretary to Council (2009-2013); and Acting Deputy Vice Chancellor- Research and Knowledge Exchange (2013 to date). Besides, Prof. Luoga is an advocate of the High Court of Tanzania.

Prof. Luoga researches and publishes widely in the areas of taxation, human rights, law and procurement.

No comments

+255716829257