VIDOKEZO MUHIMU VYA KUPATA KAZI..
Fahamu
njia mbalimbali za kupata kazi Tanzania, pitia tovuti na blogu kama njia rahisi
ya kupata taarifa juu ya nafasi za Ajira Tanzania, fahamu yote haya kupitia chimbuko blog.
Vidokezo vya namna ya kutafuta na
kuomba kazi Tanzania
Napataje kazi Tanzania?
Ukiwa Tanzania unaweza kutafuta kazi
kwa kutumia njia zifuatazo:
• Kupitia vyombo
vya Habari; kwa mfano magazeti, tovuti na blogu ambazo ni mashuhuri kwa
kutangaza matangazo mbalimbali.
• Kwa kupitia mara
kwa mara tovuti za makampuni ambayo ungependa kufanya nao kazi. Makampuni mengi
huweka matangazo ya nafasi za kazi katika tovuti zao na sio lazima katika
magazeti. Ni muhimu kua na mazoea ya kutembelea tovuti mbalimbali mara kwa
mara, hii itaongeza nafasi yako ya kupata kazi.
• Kupitia marafiki
na jamaa ambao wanaweza kukupatia taarifa muhimu kuhusu nafasi za kazi na pia
kukushauri wapi pa kupeleka maombi ya nafasi za kazi.
• Kwa kutumia
mawakala wa kuajiri kama vile Radar Recruitment, Kazi Services Ltd na wengineo.
Kwa kawaida mawakala hawa hua na tovuti ambazo mtu hujiandikisha na kutuma CV
yake kwa mtandao baada ya kuchagua aina za kazi ambazo ungependelea kufanya.
Kumbuka kuweka mawasiliano yako ili kukuwezesha kupata nafasi.
• Tembelea pia
mawakala wa ajira wa Taifa kama vile TeSA ( Wakala wa huduma za ajira Tanzania)
kwa taarifa juu ya nafasi za kazi zilizopo.
• Pia waweza
tembelea moja ya makampuni ambayo ungependa kufanya kazi na kuomba kuongea na
meneja rasilimali watu au hata Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni pale
inapowezekana. Unaweza kutuma barua ya kuomba kazi pamoja na CV yako kwa
makampuni haya. Hii inaweza kua njia mbadala kwa kuzingatia kwamba mara nyingi
inakua ngumu kuwaona hawa watu.
Ni vipi nitaomba kazi?
Ni vipi nitaomba kazi?
Unapokua na taarifa za kutosha
juu ya uwepo wa nafasi za kazi ambazo zinakidhi sifa zako au unataka kuomba
hata bila ya kutangazwa kumbuka kufanya yafuatayo:
• Tuma barua ya
kuomba kazi yenye taarifa muhimu kama ilivyoelezwa katika dokezo la kuandika
barua za kuomba kazi. Barua hii iambatanishwe na CV ili kuweza kumpatia mwajiri
mtarajiwa taarifa zote za muhimu kukuhusu. Ukimaliza haya subiri kwa kipindi
Fulani, mara nyingi utaitwa kwenye usahili.
• Hakikisha
unatuma barua na CV yako katika anuani sahihi. Anuani hizi hutolewa wakati
nafasi za kazi zinavyotangazwa au pia unaweza kupata katika tovuti ya kampuni
husika au hata katika vipeperushi vya kampuni husika. Kama nafasi haikutangazwa
unaweza kupiga simu kufuatilia kama walipokea maombi yako na kama kuna
utaratibu wowote unaoendelea.
• Hakikisha CV
yako ni fupi na yenye taarifa zote muhimu zinazohitajika. Taarifa hizi ni
muhimu zikawepo katika ukurasa wa kwanza wa CV yako.
• Tengeneza barua
yako kwa kuweka msisitizo katika ujuzi ambao unawiana na mahitaji ya kazi
iliyotangazwa.
• Andaa makabrasha
yako yote yatakayosindikiza maombi yako kama vile, vyeti vya shule na barua za
wadhamini. Ni vizuri ukawa na nyaraka hizi katika mfumo wa picha kwa kuscan
ilikukuwezesha kufanya maombi kwa kupitia mtandao. Kama utascan hakikisha unahifadhi
nyaraka zako katika mfumo wa PDF.
Kutuma maombi yako kwa barua pepe
• Hakisha unatumia
anuani yako binafsi ya barua pepe au ya mtu wako wa karibu sana, hii itasaidia
katika kupata majibu kwa wakati.
• Kila mara tuma
barua, CV na vyeti vyako kama ujumbe mmoja wa barua pepe na viambatanisho
vyake. Ni vizuri kua na orodha ya vitu vyote muhimu unavyotakiwa kufanya wakati
wa kutuma maombi ya kazi. Soma tena na tena kuepuka makosa. Kabla hujabonyeza
kitufe cha kutuma soma tena kuepuka makosa.
• Ukishatuma subiri majibu
sasa. Hakikisha namba yako ya simu na njia nyingine za mawasiliano ulizoweka
katika CV yako zinapatikana wakati wote toka utume maombi yako.
No comments
+255716829257