Habari mpya

NI HAKI ZIPI ZA WAFANYAKAZI WA NDANI ZINAZOLINDWA NA AZIMIO JIPYA LA SHIRIKA LA KAZI LA KIMATAIFA?

Image result for SHIRIKA LA KAZI LA KIMATAIFA nembo
Maazimio mapya yanasisitiza upatikanaji wa haki za msingi kwa wafanyakazi wa ndani kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine. Zaidi ya hayo pia inasisitiza kwamba:
1.    Wafanyakazi wa ndani wafahamishwe juu ya sheria na kanuni za ajira katika njia inayoeleweka kupitia mikataba ya maandishi;

2.    Wafanyakazi wa ndani wafanye kazi katika muda wa kazi wa kawaida ( kwa mfano, saa 45 kwa wiki kwa Tanzania) na vielelezo vingine kama malipo ya kufanya kazi muda wa ziada, mapumziko ya siku, wiki pamoja na likizo ya mwaka yenye malipo yazingatiwe;

3.    Kima cha chini cha mshahara na umri wa chini wa kuajiriwa kwa kuzingatia kanuni za sheria za kazi za nchi.

4.    Mishahara ilipwe yote kamili, ijapokua kiasi kidogo cha malipo kinaweza kua katika njia nyingine.

Kwa wafanyakazi wa ndani waliohamia, maazimio yanasisistiza kuwepo mkataba wa maandishi utakao tiwa sahihi na kukabidhiwa kwa mfanyakazi kabla hajavuka mipaka ya nchi. Hata hivyo maazimio haya hayatatumika kama tayari kuna makubaliano ya pamoja baina ya nchi. Maazimio haya pia hayatatumika na Umoja wa Ulaya (EU)

No comments

+255716829257