Habari mpya

JIFUNZE KILIMO BORA CHA NYANYA

Image result for JIFUNZE KILIMO BORA CHA NYANYA\
Nchini Tanzania zao la nyanya hulimwa karibu katika mikoa yote hasa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mwanza, Dodoma, Tanga, Pwani na Mbeya.
Nyanya hutupatia vitamini A, B, na C. Vile vile zina madini aina ya chuma na chokaa.
MATUMIZI:
Nyanya hutumika kama kiungo cha kupikia. Huweza kuliwa mbichi kama kachumbari au zikiwa zimekaangwa pamoja na nyama au mboga yoyote. Nyanya pia zinaweza kutengenezwa supu, vinywaji, achari, jemu, sosi na pesti. Vilevile zinaweza kukatwa katwa vipande na kuhifadhiwa kwenye makopo. Mabaki ya mimea hutumika kama mbolea na chakula cha wanyama.
MAZINGIRA:
Nyanya hustawi katika udongo wa aina nyingi ili mradi uwe mwepesi na usiotuamisha maji. Udongo unaofaa zaidi ni ule wa kitifutifu na wenye mboji nyingi. Hali kadhalika udongo wenye uchachu wa wastani m mzuri kwa kilimo cha zao hili.
Joto lifaalo kwa ustawishaji wa nyanya ni kutoka nyuzijoto 18 hadi 30 za Sentigredi. Joto likizidi husababisha matawi ya matunda kuwa machache. Vilevile joto jingi, mwanga kidogo, pamoja na hali ya unyevunyevu husababisha magonjwa mengi kuenea na mmea kuwa na majani mengi na matunda kidogo. Joto kidogo hufanya mimea kutoa matawi mengi na matunda madogo ambayo huchelewa kukomaa.
Zao hili hupendelea mvua za wastani pamoja na kipindi kirefu chajua. Hali ya mvua nyingi pamoja na baridi kali husababisha kuenea kwa magonjwa na wadudu waharibifu.
AINA:
Aina nzuri za nyanya ni zile zinazotoa mavuno mengi na bora; zinazostahimili magonjwa, zinazokomaa mapema, zenye ladha nzuri na umbo la kuvutia,. Zifuatazo ni aina bora za nyanya zinazolimwa hapa nchini; Aina hizi zimegawanyika katika makundi makuu mawili kutegemea ukuaji wake;
· Aina fupi:- Dwarf germ, Cal - J, Amateur, Red Cloud, Roma, Reza na Columbian.
· Aina ndefu:- Money Maker, Marglobe, Beef Master, Lot No 2009, Mandel, Tengeru 97 na Tanya.
KUOTESHA MBEGU:
Mbegu za nyanya huoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye huhamishiwa shambani. Matayarisho ya kitalu hufanyika wiki moja au mbili kabla ya kupanda mbegu. Tengeneza tuta lenye upana wa mita moja na urefu wowote. Vunja mabonge makubwa kwa kutumiajembe. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri kiasi cha ndoo moja hadi mbili katika eneo la mita mraba mmoja. Changanya mbolea hii na udongo vizuri. Sawazisha kwa kutumia reki au kifaa chochote.
Mwagilia kitalu siku moja kabla ya kupanda, kisha sia mbegu katika mistari yenye nafasi ya sentimita 10 hadi 15 kutoka mstari hadi mstari Kiasi cha mbegu kitakachotosha eneo hilo la mita mraba moja ni gramu tatu hadi tano (sawa na nusu kijiko cha chai mpaka kijiko kimoja). Kiasi hiki cha mbegu huweza kutoa miche inayoweza kutosha kupandikiza katika eneo la mita mraba 100. Kiasi cha mbegu kinachohitajiwa kwa hekta moja ni gramu 300 hadi 500.
Weka matandazo kama vile nyasi kavu au majani ya migomba kisha mwagilia maji asubuhi najioni mpaka mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku tano hadi 10. Ondoa nyasi mara baada ya mbegu kuota na endelea kummwagilia hadi miche itakapohamishwa. Jenga kichanja ili kuzuiajua kali na matone ya mvua yanayoweza kuharibu miche michanga.
KUTAYARISHA SHAMBA:
Matayarisho ya shamba yaanze mwezi mmoja kabla ya kupandikiza. Katua ardhi katika kina cha kutosha hadi kufikia sentimita 30. Lainisha udongo kwa kuvunja mabonge makubwa kwa kutumiajembe.
Weka mbolea za asili wiki mbili kabla ya kupandikiza. Kiasi kinachohitajika m tani 20 kwa hekta (sawa na ndoo moja hadi mbili) kwa kila eneo la mita mraba mmoja. Mbolea hii iwekwe katika kila shimo la kupandia na ichanganywe vizuri pamoja na udongo.
KUPANDIKIZA:
Upandikizaji wa miche shambani hufanyika baada ya wiki nne hadi sita kutegmea hali ya hewa. Siku 10 hadi 14 za mwisho kabla ya kupandikiza, izoeshe miche hali ngumu ambayo inalingana na ile ya shamba la kudumu. Wakati huu ipatie miche maji kidogo na iondolee kivuli. Mwagilia kitalu siku moja kabla ili kurahisisha ung'oaji wa miche na kuepuka kukata mizizi. Pia ni muhimu kumwagilia shamba siku moja kabla ya kupandikiza. Iwapo mbolea za asili hazikutumika wakati wa kutayarisha shamba unashauriwa kuweka mbolea ya mchanganyiko (N.P.K. 5:10:5) kiasi cha gramu tano kwakilashimo wakati wa kupandikiza.
Pandikiza miche wakati wa asubuhi aujioni ili kuepukajua kali linaloweza kunyausha miche. Wakati wa kupandikiza hakikisha mizizi haipigwi na jua, kwa kuiweka katika ndoo au chombo chochote chenye udongo wenye unyevu. Pandikiza miche katika kina cha sentimita mbili hadi tatu zaidi ya ilivyokuwa kwenye kitalu ili kupata mizizi mipya. Kisha shindilia udongo vizuri kuzunguka mche na mwagilia maji.
Nafasi:
Nafasi zinazotumika hupandikiza miche shambani hutegemea aina ya nyanya, njia ya kumwagilia na hali ya hewa, kwa mfano:-
Aina fupi ya nyanya hupandikizwa katika nafasi ya sentimita 90 kutoka mstari hadi mstari, na sentimita 50 kutoka mche hadi mche. Nafasi kati ya tuta na tuta iwe sentimita 60. Aina hii haihitaji kuegeshwa mwenye miti. Kutokana na nafasi hii jumla ya mimea 240 hadi 275 itaweza kupandikizwa katika eneo la mita mraba 100 (hatua kumi kwa kumi) ambayo ni sawa na miche 20,000 hadi 22,000 kwa hekta.
Aina ndefu ya nyanya inayohitaji kuegeshwa kwenye mti hupandikizwa katika nafasi zifuatazo:-
· Kupandikiza Safu Mbili Katika Tuta Moja
Kutoka mstari hadi mstari ni sentimita 75 na mche hadi mche ni sentimita 50 hadi 60. Aina hii inahitaji kuegeshwa kwenye miti. Jumla ya mimea 220 hadi 275 inaweza kupandikizwa katika eneo la mita mraba 100 ambayo ni sawa na miche 18,000 hadi 22,000 kwa hekta.
· Kupandikiza Safu Moja Katika Tuta Moja;

Nafasi kati ya tuta na tuta ni sentimita 90 na kutoka mche hadi mche ni sentimita 40 mpaka 50. Jumla ya mimea 220 hadi 275 inaweza kupandikizwa katika eneo la mita mraba 100.
KUTUNZA SHAMBA:
Kuweka Matandazo:
Baada ya kuhamishia miche shambani, weka matandazo ili kuhifadhi unyevu na kuzuia magugu. Matandazo pia husaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo na kutunza rutuba. Vile vile hupunguza uzito wa matone ya mvua na kuweka matunda katika hali ya usafi.
Kusimika Miti na Kuegesha Mimea:
Kazi ya kusimika miti na kuegesha mimea hufanyika wiki ya pili baada ya kupandikiza. Miti ya kuegesha mimea iwe imara, na ambayo haiozi haraka. Simika miti kiasi cha umbali wa sentimita tano kutoka kwenye mmea. Wakati wa kusimika mti hakikisha kwamba mmea unakuwa upande wa ndani ili kuzuia mmea usiumie wakati wa kuchuma au kunyunyuzia dawa. Kisha kwa kutumia mkono shindilia mti sentimita 20 hadi 50 kwenda chini ya ardhi. Mti uwe na urefu wa mita moja na nusu hadi mbili na unene wa sentimita mbili hadi tatu.
Kufunga Nyanya Kwenye Mti:
Aina ndefu ya nyanya ni lazima ifungiwe kwenye mti ili kuzuia mmea usitambae chini. Mimea iliyofungwa kwenye mti hurahisisha unyunyiziaji wa dawa, umwagiliaji na uchumaji wa matunda. Ili kupata mazao yaliyo bora na makubwa ondoa matawi yote na kuacha mashina mawili. Yafungie mashina hayo kwenye mti ili mimea iweze kutambaa na kuwa wima. Funga kamba katika umbo la nane chini ya kila jani la tatu na kila baada ya sentimita 20 hadi 25.

Aina ndefu za nyanya hutoa mavuno mengi kama zitawekewa miti, zitapunguziwa matawi, majani na mizigo ya matunda
Kupunguza Matawi
Kupunguza matawi ni muhimu na hasa kwa aina ndefu kama vile Money Maker. Kazi hii hufanyika mara moja kwa wiki. Wakati mzuri wa kupunguzia ni asubuhi. Ondoa matawi yote na acha shina moja au mawili. Usitumie kisu kupunguzia matawi hali matawi yavunjwe kwa kutumia mkono. Utumiaji wa kisu hueneza magonjwa yanayosababishwa na virusi au baktena
Kuondoa Majani:
Ondoa majani yote yanayoonyesha dalili za magonjwa au kushambuliwa na wadudu na yale yote yaliyozeeka ili kupunguza hali ya unyevu na kuruhusu hewa ya kutosha kwa mimea. Ondoa majani mawili au matatu yaliyo chini ya ngazi ya kwanza ya matunda kisha yachome au yafukie
Kukata Kilele:
Kwa kawaida aina ndefu ya nyanya huzaa ngazi zaidi ya sita za matunda, lakini mmea una uwezo wa kubeba ngazi tano hadi sita tu. Hivyo ni muhimu kukata sehemu yajuu ya mmea (kilele) ili kusimamisha ukuaji wake. Kata kilele mimea ifikiapo ngazi hizo. Jani moja liachwe juu ya ngazi ya mwisho (ya tano au ya sita).
Machipukizi yote yanayojitokeza pembeni hayana budi kuondolewa ili kupata matunda makubwa na yatakayoiva upesi.
Palizi:
Palizi katika shamba la nyanya ifanywe kwa uangalifu ili kuepuka kukata mizizi. Punguza palizi ya mara kwa mara kwa kuweka matandazo kuzuia uotaji wa magugu. Wakati wa kupalilia, pandishia udongo kwenye shina.
Kumwagilia:
Kwa kawaida nyanya hutoa mavuno mengi wakati wa kiangazi kuliko wakati wa masika. Mwagilia maji ya kutosha mara mbili kwa wiki hasa matunda ya kwanza yanapoanza kutunga. Kumwagilia maji mengi sana au kidogo sana kunasababisha matunda yawe na hitilafu ya kupasuka. Wakati wa mwanzo epuka kumwagilia maji mengi ili mimea isididimie.
Kuweka Mbolea ya Kukuzia:
Mbolea ya kukuzia howekwa mara mbili. Mara ya kwanza weka gramu tano za S/A auCAN kwa kila mche katika wiki ya pili hadi ya nne baada ya kupandikiza. Rudia tena kuwekakiasi hicho hicho wakari matunda ya ngazi ya kwanza yanapoanza kuiva.
Wadudu na Magonjwa:
Wadudu Waharibifu:
· Funza wa Vitumba (American Bolfworm):
Hawa m funza watokanao na aina fulani ya nondo. Funza hawa wenye rangi ya kijani hutokea baada ya mayai ya nondo kuanguliwa. Kisha hutoboa matunda na kuishi humo. Jinsi wanavyokula na kukua husababisha matunda kuoza. Wadudu hawa wanazuiwa kwa kunyunyizia dawa kama vile Carbaryl naDimethoatekilabaadayasikunnehadisaba. Dawanyingine zinazoweza kutumika ni Ekalux, Karate, Fenvalerate, Deltamethrin na Pennethrin.
· Inzi Weupe (White flies):
Wadudu wadogo wapevu na wamefimikwa na vumbi jeupe kama unga. Hufyonza utomvu chini ya majani na kuifanya mimeaidumae. Vilevilehuenezamagonjwayanayosababishwa na virusi. Dawa zinazozotumika kuzuia wadudu hawa ni Dimecron, Fenvalcrate (Sumicidin) na Dichlorvos.
· Utiliri (Red Spider Mites):
Hivi ni vijidudu vidogo na vyenye rangi ya machungwa yaliyoiva, nyekundu, au kikahawia. Vijidudu hivi hushambulia kwa kufyonza utomvu chini ya majani. Majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya njano, hukunjamana, hukauka na hatimaye mmea hufa. Zuia utitiri kwa kutumia dawa kama vile Morestan, Kelthane, Karathane, Dimethoate, Diazinon, Ekalux, Politrin, na Profenofos.
· Vidukari/Wadudu Mafuta (Aphids):
Ni wadudu wadogo wenye rarigi ya kijani, nyeusi au kikahawia. Baadhi yao wana mabawa na wengine hawana. Hufyonza utomvu wa majani na kusababisha mmea ulioshambuliwa kudhoofika, kudumaa, majani kunyauka na hatimaye kukauka. Wadudu hawa huangamizwa kwa kutumia moja ya dawa zifuatazo:- Dimecron, Actellic 50 EC, Selecron, Fenvalerate (Sumicidin), Karate, Dichlorvos na Dimethoate.
· Minyoo Fundo (Rootknot Nematodes):
Ni wadudu weupe wadogo wanaoishi ardhini ambao hawaonekani kirahisi kwa macho. Hushambulia mizizi na kuifanya mimea kudhoofika na kushindwa kutoa matunda. Vile vile husababisha matunda kuiva kabla ya kukomaa. Uking'oa mmea ulioshambuliwa utaona mizizi ina nundunundu. Zuia minyoo fundo kwa kubadilisha mazao. Baada ya kuvuna nyanya, zao linalofuata lisiwe lajamii yake kwa mfano pilipili na bilinganya. Kama madhara m makubwa sana, tumia Furadan au dawa za kufukiza ardhi kama vile Dazomet, na Curaterr.
KUMBUKA:
Kumwagilia kwa kutumia mifereji kunaweza kusambaza minyoo shambani.
· Sota (Cutworms):
Hawa ni funza wakubwa wenye rangi ya kijivu. Hupendelea kujichimbia katika udongo wakati wa mchana na hujitokeza wakati wa usiku au asubuhi sana kukata miche michanga karibu na usawa wa ardhi.
Zuia wadudu hawa kwa kutumia majivu au dawa kama vile Carbaryl (Sevin), Fenvalerate (Sumicidin) na Deltamethrin (Decis) mara baada ya kupanda. Kama mche utakatwa mtoe mdudu kwa kumfukua na kumwuua kisha pandikiza mche mwingine.
Njia nyingine ya kumzuia mdudu huyu ni kuweka shamba na mazingira yake katika hali ya usafi ili wasiweze kuzaliana kwa wingi. Ikiwezekana tifua udongo bila ya kupanda zao lolote kwa muda wa mwezi mmoja.
Magonjwa:
· Magonjwa ya Bakajani (Early and Late Blight):
Magonjwa haya husababishwa na ukungu. Hushambulia majani, shina na matunda.
· Bakajani (Early Blight):
Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana kwenye kingo na pembe za majani. Kingo za majani huwa na madoa ya rangi nyeusi iliyochanganyika na kikahawia. Pembe zake huwa za njano. Shina huwa na madoa yanayofanana na yale yanayotokea kwenye majani lakini huwa yamesambaa na kuonekana zaidi. Baadaye madoa haya hupanuka na kuwa mabaka makubwa yenye rangi nyeusi. Kwa kawaida mabaka haya huwa makavu na yaliyodidimia. Ugonjwa ukizidi mmea hudumaa na huvunjika kwa urahisi.
Matunda huwa na madoa meusi ya mviringo. Madoa haya huonekana zaidi kwenye kikonyo cha tunda na kwenye sehemu iliyopasuka. Kadri tunda linavyozidi kuiva, madoa haya huongezeka zaidi.
· Bakajani (Late Blight):
Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana kwenyejani la chini. Maj ani na shina huwa na mabaka makubwa yenye rangi nyeusi au kikahawia nzito. Katika sehemu zenye hali ya hewa ya unyevunyevu, majani huoza na hatimaye uyoga mweupe huonekana chini ya jani. Majani haya baadaye hukauka na kuwa kama yaliyounguzwa na moto.
Matunda yaliyopatwa na ugonjwa huu huwa na madoa ya rangi ya kijani iliyochanganyika na kikahawia. Baadaye madoa haya huwa makubwa na hatimaye huoza. Ukipasua tunda lililoathiriwa utaona weusi. Nyanya zenye ugonjwa huu zikihifadhiwa kwenye sehemu yenye unyevu mwingi hutoa uyoga mweupe. Magonjwa ya bakajani yanazuiwa kwa kuzingatia yafuatayo:-
- Kubadilisha mazao
- Kuweka matandazo shambani.
- Kupanda aina ya nyanya zinazovumilia mashambulizi ya magonjwa haya.
- Kuweka shamba katika hali ya usafi kwa kuondoa masalia ya mazaoshambani baada ya kuvuna.
- Kupunguzia matawi na kuondoa majani yote yaliyoshambuliwa.
- Kupanda mbegu kwenye kitalu kilichotayarishwa vizuri.
- Kutumia dawa za ukungu kama vile Dithane - M 45, Ridomil, Topsin M 70, Cupric Hydroxide (Champion) na Copper Oxychloride (Cupro).
· Mnyauko Bakteria (Bacterial Wilt):
Ugonjwa huu husababishwa na vijidudu vya bakteria. Mmea ulioshambuliwa na ugonjwa huu hunyauka ghafla hasa wakati wajua kali. Baadaye mmea hudumaa, majani na vikonyo vyake hukunjamana. Kama shina likikatwa karibu na usawa wa ardhi, rangi ya kikahawia nzito huonekana kwenye sehemu zinazosafirisha maji. Sehemu iliyokatwa ikiwekwa kwenye maji, maji yenye rangi ya maziwa huchuruzika.
Zuia ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo:-
- Kupanda nyanya kwenye sehemu ambayo haina ugonjwa huu.
- Kubadilisha mazao.
- Kuepuka kuweka mbolea nyingi ya samadi au chumvi chumvi.
- Kuotesha mbegu kwenye kitalu ambacho hakina ugonjwa huu.
- Kupanda nyanya zinazostahimili ugonjwa huu.
· Mnyauko Fuzari (Fusarium Wilt);
Huu pia ni ugonjwa wa ukungu au kuvu. Husababisha majani yawe na rangi ya njano na mmea kunyauka hasa wakati wajua kali. Majaniyaliyoshambuliwahuvunjikakwaurahisi. Kama ganda la shina likinyofolewa karibu na usawa wa ardhi, rangi ya kikahawia huonekana. Ugonjwa huu huzuiwa kwa kuzingatia yafuatayo:-
- Kupanda aina za nyanya zinazostahimili ugonjwa kama vile ROMA na VFM
- Kung'oa mimea iliyoshambuliwa na kuichoma au kuifukia.
- Kutumia dawa kama vile Topsin M 70. Dawa hii iwekwe au inyunyiziwe kwenye udongo.
· Ugonjwa wa Madoajani (Septoria Leaf Spot);
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hushambulia majani. Majani yaliyoshambuliwa huwa na madoa meusi na kingo zake huwa na rangi ya kijivu ilioambatana na madoa madogo meusi. Zuia ugonjwa kwa kunyunyizia dawa za ukungu kwa mfano Dithane - M 45, Blitox na Copper Fungicides kama vile Copper Hydroxide (Kocide), Copper Oxychloride (Cupro), na Cupric hydroxide (Champion).
· Batobato (Tobacco Mosaic Virus):
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na virusi. Hushambulia majani machanga na yaliyozeeka. Majani machanga yaliyoshambuliwa hukunjamana na kudondoka. Halikadhalika majani yaliyozeeka hukunjamana, huvunjika kwa urahisi na huwa na rangi nyeusi, kijivu au kikahawia chini ya jani. Mwishowe majani hunyauka na kufa. Ugonjwa huu unazuiwa kwa kuzingatia yafuatayo:-
- Kung'oa na kuchoma mimea yote iliyoshambuliwa
- Kupanda mbegu zilizothibitishwa kitaalam
- Kupanda aina za nyanya zinazostahimili magonjwa ya batobato
- Kuepuka kuhudumia mimea ambayo haina ugonjwa baada ya kuhudumia mimea yenye ugonjwa. Ikiwezekana osha mikono kabla ya kuhudumia mimea mingine
- Kutovuta sigara ndani ya shamba la nyanya
- Kusafisha vifaa vyote kama vile visu, mikasi kwa maji na sabuni baadaya kuvifanyia kazi.
· Tomato Yellow LeafCurl:
Ugonjwa huu husababisha majani kujifunga kuelekea ndani. Kilele cha mmea huonyesha rangi ya njano. Mmea hudumaa na baadaye hushindwa kutoa matunda mengi. Jani hupoteza umbo lake la kawaida na kuwa kama ufagio. Ugonjwa huu huenezwa na inzi weupe, hivyo zuia wadudu hawa kwa kutumia dawa kama vile Fenvalerate, Dichlorvos, na Dimecron. Vilevile usivute sigara ndani au kando kando ya shamba.
HITILAFU ZA MATUNDA
· Kupasuka Matunda:
Kuna aina mbili za mipasuko; Mpasuko wa mviringo na mpasuko wa nyota.
· Mpasuko wa Mviringo:
Hali hii hutokea wakati mmea haukupata maji ya kutosha hasa wakati wa jua kali. Wakati huu maji yaliyoko kwenye tunda hayawezi kulingana na maji yanayopotea angani kama mvuke.
· Mpasuko wa Umbo la Nyota:
Hutokea hasa tunda linapokuwa na maji mengi na wakati huo unyevu angani ni mwingi sana. Hivyo tunda hushindwa kupoteza maji kwa njia ya mvuke na hupasuka kabla ya kukomaa. Hutokea zaidi kwenye nyanya aina ya Marglobe. Mpasuko wa mviringo na wa umbo la nyota huzuiwa kwa kumwagilia maji inavyotakiwa.
· Kuoza Kitako:
Vidonda vyeusi vilivyodidimia huonekana kwenye kitako cha tunda. Sehemu hii baadaye hunyauka na ngozi huwa nyeusi. Hali hii hutokea zaidi wakati wa jua kali na katika sehemu zenye udongo wenye chumvi na tindikali nyingi.
Zuia hali hii kwa kuhakikisha udongo unaunyevu wa kutosha wakati wote. Pia epuka kuweka mbolea nyingi za chumvi chumvi.
· Mabaka ya Matunda:
Matunda yaliyopigwa najua kali huwa na mabaka hasa sehemu za ubavuni. Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kuepuka kupunguza matawi mengi kwa wakati mmoja.
· Matunda ya Kijani Kibichi:
Mabega ya tunda huwa na rangi ya kijani kibichi. Hitilafu hii hutokana na chanikiwiti (chlorophyll) kuwa nyingi na hutokea hasa wakati wa jua kali. Ili kuepuka hali hii unashauriwa kutokuweka mbolea nyingi ya chumvi chumvi na punguza mwanga wa jua kwa kufunika matunda na majani makavu.
KUVUNA:
Zao la nyanya huwa tayari kwa kuvunwa baada ya wiki 14 hadi 16 tangu kuotesha mbegu. Kwa kawaida aina fupi huchukua muda mfupi kukomaa kuliko aina ndefu. Uvunaji huchukua muda wa wiki sita hadi nane. Aina ndefu huchukua muda mrefu kuvuna kuliko aina fupi. Uchumaji hufanyika mara mbili au tatu kwa wiki kutegemea aina, usafiri, mahali pa kuhifadhi na mahitaji ya soko. Nyanya kwa ajili ya matumizi ya nyumbani huvunwa wakati zimeiva kabisa. Nyanya kwa ajili ya kusafirisha au kuhifadhiwa kabla ya matumizi huchumwa kabla ya kuiva sana. Wakati huo huwa bado na rangi kati ya Idjani na njano. Chuma nyanya kwa uangalifu sana. Nyanya zivunwe na vikonyo vyake kwani huwezesha tunda kuendelea kuiva vizuri na husaidia nyanya zisioze haraka.
Chombo cha kuvunia kiwe imara na kiwe na uwezo wa kuingiza hewa ya kutosha.
Iwapo mimea ya nyanya itatunzwa vizuri, inaweza kutoa mavuno kiasi cha tani 25 hadi 60 kwa hekta.
KUPANGA NYANYA KATIKA DARAJA:
Nyanya zikishavunwa hupangwa katika daraja kufuata ubora wa tunda, ukubwa na rangi yake.
Kupanga Kufuata Ubora wa Tunda:
Ondoa nyanya zote zilizo mbovu, zenye kushambuliwa na wadudu au magonjwa kabla ya kuamua kuchagua zitakazosafirishwa au kuhifadhiwa. Nyanya zilizofanyiwa uchaguzi mzuri hupata bei nzuri zikiuzwa katika masoko makubwa.
Kupanga Kufuata Rangi ya Tunda.
Ni muhimu kupanga nyanya kufuata rangi. Kupanga nyanya kufuata rangi husaidia kupata nyanya zenye usawa wa kukomaa. Katika kupanga kufuata rangi, panga ifuatavyo:-
- Nyanya zilizokomaa zenye rangi ya kijani kibichi.
- Nyanya zilizoiva zenye rangi ya pinki.
- Nyanya zilizoiva zenye rangi nyekundu.
KUFUNGASHA:
Nyanya kwa ajili ya kusafirisha zinatakiwa ziwekwe kwenye visanduku vya mbao vidogo dogo visivyozidi ujazo wa ndoo mbili.
KUUZA NA KUHIFADHI
Nyanya ni bidhaa zinazoharibika haraka, hivyo ni muhimu zifikishwe kwa mlaji mapema baada ya kuchumwa. Kama inawezekana kupata vyombo vya kuleta hali ya ubaridi inafaa kuhifadhi na kusafirisha katika hali ya ubaridi ipatayo nyuzijoto 12 za Sentigredi. Katika hali hii nyanya zinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
KUBADILISHA MAZAO:
Zao la nyanya hutumia chakula kingi ardhini. Hivyo baada ya kuvuna zao hili lisifuatwe na zao la jamii ya nyanya kama vile bilinganya, ngogwe, pilipili na viazi mviringo. Hali kadhalika zao hili lisifuatiwe na zao lingine Iplote linalotumia chakula kingi mpaka kumewekwa mbolea ya kutosha. Kubadilisha mazao hupunguza kuenea kwa wadudu na magonjwa yanayoshambulia jamii hii ya mazao. Vilevile huhifadhi rutuba ya udongo. Mfano unaofaa wa kubadilisha mazao:

(1) Nyanya, (2) Kabichi/Mchicha, (3) Vitunguu/Karoti, (4) Jamii ya Kunde. 

No comments

+255716829257