HIZI NDIO NJIA TANO KALI ZA KUPATA MTOTO WA KIUME..
Uzazi wa mpango una mambo mengi
sana.. sio kuzuia mimba tu ndio uzazi wa mpango ila hata kupanga idadi na
jinsia za watoto ni moja ya njia za uzazi wa mpango..
Watu wengi wamekua wakitamani jinsia
flani za watoto ili wazae watoto wachache ila kukosa kwa jinsia waliyoipanga
hujikuta wakizaa watoto wengi wakati wakitafuta jinsia husika, mpaka familia
hugombana na kutengana kwa sababu hizi.
Mara nyingi wazazi wa kiume hufikia
hatua ya kuvunja ndoa kabisa hasa wanapokosa watoto wa kiume.
Leo ntamaliza kitendawili hiki kwa
kutoa njia ambazo zinaweza kufanya mtu kupata mtoto wa kiume kwa asilimia
nyingi…
Kitaalamu mbegu zinazotoa
mtoto wa kiume XY huenda kwa mwendo mkali sana kwenda kwenye mfuko wa uzazi
lakini hufa haraka. lakini mbegu zinazotoa mtoto wa kike XX husafiri taratibu
na huchelewa kufika na kufa ndani ya mfuko wa uzazi kwani mbegu hizi
huweza kuvumilia hali mbaya ya kimazingira ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke,
hivyo njia pekee ya kupata mtoto wa kiume ni kuhakikisha mbegu hizo za kiumeXY
zinakutana na mayai ya kike kwenye mfuko wa uzazi haraka kabla ya kufa..
Zifuatazo ni njia hizo tano kali…
1.
Hakikisha
unashiriki tendo la ndoa siku mayai ya mwanamke yanapokua yameshuka{ovulation}
Ukishiriki tendo la ndoa siku hii ambayo yai
linakua limeshuka mbegu za kiume huweza kufika mapema na kujiunga
na mayai ya kike na kutengeneza mtoto{fertilization}hii ni siku ya
14 kabla ya kuona damu ya mwezi unaofuata sio baada ya kuona siku zako..
Kama wewe mwanamke hujui siku yako ya ovulation fanya hivi.
Pima
joto lako la mwili: nunua kipima joto[thermometer} na kisha pima joto lako kila
asubuhi , siku ukiona joto lako limeongezeka kidogo ujue umeanza ovulation na
hiyo ndio siku muhimu ya kutafuta mtoto..
Angalia maji maji ya uke: kawaida maji ya uke hua mazito na
kuvutika kama maji ya mayai mabichi wakati mwanamke anapoanza ovulation..
2. Wewe
mwanaume ongeza idadi ya mbegu zako..{sperm count}
Mwanaume anatakiwa aongeze wingi wa
mbegu zake hasa kwa kukaa siku mbili mpaka tano bila kushiriki tendo la ndoa
wakati akisubiri mwanamke wake aanze ovulation.
Njia zingine za kuongeza mbegu ni
weka
korodani kwenye hali ya ubaridi:
kawaida korodani hutengeneza mbegu nyingi wakati wa hali ya ubaridi kuliko joto hivyo mwanaume anatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, na kuwekalaptop kwenye mapaja
acha kuvuta sigara na kunywa pombe:wanaume wanaokunywa pombe na kuvuta sigara hua na mbegu kidogo sawasawa na wavutaji wa bangi..
matumizi ya dawa za cancer pia husababisha uzalishaji wa mbegu kidogo sana.
kawaida korodani hutengeneza mbegu nyingi wakati wa hali ya ubaridi kuliko joto hivyo mwanaume anatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, na kuwekalaptop kwenye mapaja
acha kuvuta sigara na kunywa pombe:wanaume wanaokunywa pombe na kuvuta sigara hua na mbegu kidogo sawasawa na wavutaji wa bangi..
matumizi ya dawa za cancer pia husababisha uzalishaji wa mbegu kidogo sana.
3. Tumia
style za ngono ambazo zinahamasisha muingilio mkubwa{deep penetration}
Hii huzipa faida mbegu za mtoto wa kiume{XY}
kufika haraka na kufanya fertilization na upande mwingine, muingiliano
mdogo{shallow penetration}husababisha mbegu kumwagwa mbali na mlango wa
mfuko wa uzazi hivyo mbegu huweza kukutana na hali ya tindikali kwenye uke
hivyo mbegu za mtoto wa kiume kufa haraka na kuziacha mbegu
zinazotoa mtoto wa kike.{XX}.
4. Hakikisha
mwanamke anafika kileleni:
Mwanamke anapofika kileleni hutoa
maji mengi ukeni ambayo hupunguza wingi wa tindikali ambayo ni adui wa
mbegu zote hasa mbegu za mtoto wa kiume XY ambazo hua haziwezi
kuvumilia hali ngumu ya kimazingira.
5. Usifanye
tendo la ndoa kabla na baada ya ovulation;
Kabla ya ovulation mbegu za mtoto wa
kiume XY hufika haraka kwenye mfuko wa uzazi kama kawaida na kukuta
mayai ya mwanamke hayajafika na kufa vivo hivyo baada ya ovulation.
No comments
+255716829257