EPUKA AJALI ZA BARABARANI KWA KUZINGATIA HAYA..
Na Ramadhani
Gidion#mswahili.
Fuata Kanuni hizi za
Uvukaji:
1. Tafuta sehemu salama
ya kuvuka
2. Simama kwenye ukingo
wa barabara
3. Angalia magari
barabarani kushoto, kulia na sehemu zote kukuzunguka, na sikiliza.
4. Kama kuna gari linakuja liache lipite
5. Wakati hakuna gari
linalokuja, vuka moja kwa moja barabara-usikimbie
6. Angalia na sikiliza
magari wakati wa kuvuka Mahali salama pa kuvukia.
Chagua sehemu unapoweza
kuona pande zote, na ambapo dereva anaweza kukuona. Kwa sababu hii, vuka
barabara vizuri mbali na kona kali yoyote. Mahali ambapo ni salama kuvuka
barabara, ni pamoja na kwenye taa za barabarani, kwenye alama za pundamilia,
kiplefti, madaraja ya waendea kwa miguu na njia za chini, au mahali alipo ofi
sa wa polisi, mwongoza kivuko cha shule au magari. Kuvuka kwenye kizingwa.
Iwapo kuna kizingwa katikati ya barabara,
tumia Kanuni za Uvukaji kuvuka hadi kwenye kizingwa na kisha simama. Tumia
utaratibu uleule kuvuka sehemu iliyobaki ya barabara. Kuvuka kwenye alama za
pundamilia. Iwapo kuna alama za pundamilia karibu zitumie. Mpe dereva muda wa
kutosha kukuona na kusimama kabla ya kuvuka.
Madereva wanatakiwa
kisheria wasimame pindi unapoanza kuvuka kwenye alama, lakini usivuke hadi
wanaposimama. Kisha vuka moja kwa moja, lakini endelea kuangalia na kusikiliza.
Kuvuka kwenye taa za barabarani. Katika baadhi ya sehemu kuna ishara za taa za
barabarani zinazoyaongoza magari wakati wa kusimama na watembea kwa miguu
wakati wa kuvuka. Wakati ishara ya mtu aliyewima mwenye rangi nyekundu
inapoonyeshwa USIVUKE. Wakati taa zikibadilika kuonyesha ishara ya “mtu
anayetembea” mwenye rangi ya kijani, angalia kuwa magari yamesimama na kisha
vuka kwa uangalifu.
Baada ya muda ishara ya
rangi nyekundu, au wakati mwingine ishara ya rangi ya kijani, inawaka ghafl a,
na hii maana yake usianze kuvuka, kwa sababu magari karibu yataanza kwenda
tena. Iwapo taa za barabarani hazina ishara maalumu kwa watembea kwa miguu,
angalia kwa makini na usivuke hadi taa nyekundu zikiwaka na magari kusimama.
Pamoja na hayo, angalia
magari yanayopinda kona. Kumbuka kuwa taa za barabarani zinaweza kuruhusu
magari kutembea kwenye baadhi ya njia wakati njia nyingine zikiwa zimesimama.
Vivuko vinavyoongozwa na polisi, askari wanaoongoza magari na waongozaji wa
shule. Iwapo kuna ofi sa wa polisi au mtu mwingine mwenye mamlaka ya kuongoza
magari, USIVUKE barabarani hadi wakuashirie kufanya hivyo.
Mara zote vuka mbele
yao. Usipande juu ya uzio. Katika sehemu nyingine uzio umewekwa ili kuwazuia
watembea kwa miguu kuvuka barabara na kuwaongoza mahali salama pa kuvukia.
Usipande juu ya uzio, au kutembea katikati yake na barabara. Vuka kwenye nafasi
iyowekwa. Kuvuka mitaa ya barabara moja na njia ya basi na baiskeli. Angalia ni
njia ipi ambayo magari yanakwenda, kisha tumia Kanuni za Uvukaji kuvuka
barabara.
Kuwa makini sana kwa sababu magari yanaweza
kuwa yanakwenda kasi sana kuliko kawaida. Usivuke katikati ya magari
yaliyoegeshwa. Iwapo utalazimika kuvuka katikati ya magari, tumia ukingo wa nje
wa magari iwapo barabara ina ukingo. Simama hapo na hakikisha kuwa unaweza
kuona sehemu zote na kuwa madereva wenye magari wanaweza kukuona. Endelea
kuvuka kwa kutumia Kanuni za Uvukaji. Usisimame mbele au nyuma ya gari lolote
lililosimama ambalo injini yake haijazimwa.
Wakati wa usiku, vuka
karibu na taa za mtaani. Iwapo hakuna taa za barabarani, alama za pundamilia au
kizingwa ambavyo unaweza kuvitumia, vuka karibu na taa za mtaani, ili madereva
waweze kukuona kwa urahisi zaidi. Vaa nguo zenye rangi inayoangaza au kung’aa
ili kufanya wengine wakuone kwa urahisi wakati wa usiku. Kamwe usivuke barabara
moja kwa moja nyuma au mbele ya basi. Usivuke barabara na basi acha mpaka lipite, ili uweze kuona pande zote
mbili za barabara vizuri. Usivuke mbele ya magari ya dharura.
Iwapo utayaona au
kuyasikia magari ya wagonjwa, magari ya kuzima moto, ya polisi au magari
mengine yoyote ya dharura yenye vimulimuli na sauti za ving’ora, usivuke
barabara mpaka yapite. Kuvuka na watoto. Watoto wadogo hawajui jinsi barabara
ilivyo hatari, na si wajuzi wa kuamua juu ya kasi na umbali. Kwa sababu ni
watoto ni rahisi kuchanganywa, na wanaweza kufanya vitu vya hatari. Usiwaache
watoto wadogo kuvuka barabara peke yao. Mara zote shika mikono yao kwa nguvu
wakati wa kuvuka. Watoto hujifunza kwa mifano, kwa hiyo wakati wote tumia
Kanuni za Uvukaji wakati wa kuvuka barabara, na waelezee.
Source: TAN ROAD.
No comments
+255716829257